Watafiti
kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na
Schumacker wakiwa wanamsikiliza kwa makini mkalimani ambaye ni ndugu
Sitayo aliyevaa (miwani ) katika warsha ya Wadau wa Jali Ardhi
iliyofanyika Chuo Cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus
Blog.
Wakwanza
kushoto ni Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anafuatilia kwa karibu Profesa
William Blake kutoka nchini Uingereza akipanda mti katika eneo la chuo
cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog
Mtafiti
kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akitoa
elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku
mbili wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mtafiti
kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi
akitoa elimu
kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili
wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
Profesa Willium Blake akifuatilia
kwa makini kinachoendelea katika Warsha hiyo.Picha na Vero Iganatus
Blog.
Zoezi la upandji Miti likiwa
likiendelea kwa wageni kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na
Schumacker wakishirikiana na Dkt Kelvin Kimei (anayeandika
)kutoka Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha
.Picha na Vero Ignatus Blog.
Pichani
Dkt Kelvin Kimei akimuelekeza mmoja wa wageni kutoka nchini Uingereza
namna ya kuotesha mti ikiwa ni kumbukumbu ya kutunza mazingira katika
Chuo cha Ualimu Monduli. Picha na Vero Ignatus
Blog.
Mtafiti
kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi
akitoa elimu
kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili
wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus
Blog.
Profesa
Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela Arusha akiwa anatoa ufafanuzi wa jambo katika warsha ya
Mradi wa Jali
Ardhi kwa wadau waliohudhuria katika Chuo Cha Ualimu
Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
Profesa William
Blake kutoka nchini Uingereza
akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa warsha ya siku mbili
iliyowakutanisha wadau wa Mradi
wa Jali Ardhi aliyesimama kushoto kwake ni Charles Bonaventure kutoka
Taasisi isiyo ya kiserikali ya ECHO.Picha na Vero Ignatus
Blog.
Na.Vero Ignatus, Monduli
Wananchi
wa monduli wameaswa kulima kilimo cha uhifadhi ili kuhifadhi mazingira na kuepusha kutokea
kwa mmomonyoka
wa ardhi katika maeneo yao na kudhibiti makorongo yakiwa
katika hatua za
awali.
Hayo
yamesemwa na
Issakwisa Ngondya mtafiti
kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha ambapo amesema kuwa
zaidi ya asilimia
50 katika wilaya ya Monduli imeathiriwa na mmomonyoko wa ardhi
.
Ameainisha vijiji
vilivyoathirika zaidi ni
pamoja na Emaerete,Lendikinya,Arkaria,Orchoropus ,Likamba,Oletushora pamoja na
Nangungwa,amesema kutokana na uharibifu huo wa ardhi
umesababisha rutuba kupotea katika ardhi na husababisha upatikanaji hafifu wa
mazao kwa mkulima.
Amewataka wadau hao
kuhifadhi uoto kwa
kuotesha mimea na miti
ili kuzuia udongo usisombwe na maji au upepo kwani ardhi iliyofunikwa
ni madhubuti zaidi dhidi ya mmomonyoko wa udongo kuliko ardhi ambayo
haijapandwa kitu amesisitiza kupanda mazao ya kudumu na kupanda mazao
yanayofunika ardhi.
Nae Profesa
William Blake
kutoka nchini Uingereza
amesema kuwa amefurahishwa sana na matumaini makubwa waliyonayo wana
Monduli kwaajili ya
kurudisha ardhi liyokuwa imeharibika kwa mafanikio makubwa kwani warsha
hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watu wote wa sasa na kwa vizazi vijavyo
pia
Kwa upande wake Profesa
Patrick Ndakidemi
amesema akiona mashamba
yameharibika huwa anajisikia vibaya kwani bila ardhi hakuna maisha amewataka
washiriki wote kuyatendea kazi yale yote waliyojifunza ambapo
amewataka wadau hao kuwa mfano bora katika maeneo
yao.
Akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya serikali Afisa
kilimo na ushirika na umwagiliaji Ridhiwani kombo kutoka
halmashauri ya Monduli
amewashukuru waliofanya utafiti na kurudisha majibu kwani wengine huwa
wanafanya utafiti lakini hawarudishi majibu,amesema utafiti walioufanya
utatumika katika maeneo mengine hapa nchini.
No comments:
Post a Comment