Siku chache baada ya rais kufanya ziara mkoani Tabora alipoagiza uongozi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanapambana na uharifu na watu wanaotumia silaha za moto katika matukio hayo, baadhi ya watu wametelekeza silaha za moto aina ya Magobore 12 katika wilaya za Sikonge na Kaliua ambayo yanadhaniwa kutumika katika uharifu.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi mwandamizi, SACP Willibroad Mtafungwa, ambapo amesema kuwa, kutelekezwa huko kumetokana na mwitikio wa uhamasishaji wa amani na utulivu uliofanya na kamanda wa polisi katika kata mbali mbali mkoani Tabora.
Aidha kamanda wa polisi Wilibroad Mtafungwa amesema kuwa, pamoja na kutelekezwa kwa magobore hayo bado msako utafuata kwani bado kuna watu ambao wanatolewa taarifa za kuimailika silaha ambapo amekamatwa mwanamke aliyekuwa ameficha silaha ya mmewe, aliyefungwa kutokana na uhalifu.
Kutokana na matukio hayo kamanda Willibroad Mtafungwa ametoa rai kwa jamii kutoa taarifa za siri ili watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria watiwe mbaroni.
No comments:
Post a Comment