Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Bi Julieth Binyura, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri wilaya ya Sumbawanga,achunguze tukio la mtumishi mmoja wa kituo cha afya cha Laela,la kumkatili na kumnyima dawa mwanamke mmoja akiwa na mtoto wake mchanga kinyume cha sera za afya nchini,na kumchukulia hatua kali za kinidhamu.
Mkuu huyo wa wilaya Bi Julieth Binyura aliyekuwa akikaimu ukuu wa wilaya ya Sumbawanga,ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akikabidhi vitanda vya wagonjwa ishirini na magodoro yake,vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli,na kusema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi,kuwa wanawake wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wamekuwa wakitozwa fedha kinyume cha sera za afya nchini.
Wakipokea vitanda hivyo pamoja na mashuka yake maalumu kwa ajili ya wazazi na mwana,licha ya diwani wa kata ya laela Bw Conrad Sangu kuzungumzia juu ya tatizo kubwa la maji linaloukabili mji mdogo wa Laela ikiwa ni pamoja na kituo hicho cha afya,lakini akina mama wameupokea kwa furaha kubwa msaada huo wa vitanda,na kwamba utawaondolea adha kubwa ya kulala kitanda kimoja wagonjwa wawili hadi watatu.
Chanzo: ITV Tanzania
No comments:
Post a Comment