Golden Gate, Jerusalem Golden gate ni geti kuu la mashariki lakuingilia jiji la Jerusalemu, kwa mujibu ya imani za wayahudi wanaamini kwamba mkombozi Messiah atakuja kuwakomboa na ataingia Jerusalemu akipitia kwenye geti hilo.
Ili kuzuia jambo hilo mwaka 810 Waislamu waliouteka mji wa Jerusalem walilifunga geti hilo ili Masihi asiingie, mwaka 1102 wapiganaji wa Crusade walilifungua tena baada ya kuuteka mji huo, mwaka 1187 Sultani Saladin wa Misri na Syria alilifunga tena geti hilo ili kufanikisha zoezi la kumzuia Masihi asiingie.
Baada ya Jerusalem kuangukia mikononi mwa Sultan Suleiman wa Himaya ya Ottoman aliamua kulijenga upya lakini baadaye aliamua kuliziba moja kwa moja kwa lengo lile lile la kumzuia Masihi na Nabii Eliya wasiingie Jerusalem kama wayahudi wanavyoamini. Geti hilo limezibwa mpaka leo.
Imeandaliwa na Moses Mutente
No comments:
Post a Comment