Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe, Pascal Haonga, amekamatwa na Polisi mchana huu katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi.
Mbunge huyo anahojiwa na polisi na sababu za kukamatwa kwake bado hazijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, amethibitisha kumshikilia Haonga lakini hakutaka kueleza suala hilo kwa kina kwa madai yupo nje ya ofisi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Songwe, Meshack Mgaya amesema wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu juu ya tukio hilo na baadae chama kitatoa tamko baada ya kujiridhisha sababu za kukamatwa kwa Mbunge huyo.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment