HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » Kesi ya Halima Mdee Yaahirishwa Hadi Septemba 12

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kupitia kwa Mawakili wake amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi yake ya kumtolea lugha chafu Rais Magufuli.

Mawakili watano wa Halima Mdee, wakiongozwa na Hekima Mwesigwa wamewasilisha pingamizi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya Wakili wa Serikali Leonard Chalo kudai shauri hilo limekuja kwa ajili ya kitajwa.

Mwesigwa amedai kuwa wana mapingamizi mawili, kwanza hati ya mashtaka ina mapungufu, pia Mahakama hiyo haina mamlaka akisema kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kwa sababu, Mkuu wa Wilaya aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Mdee ameshindwa kufuata matakwa ya kisheria.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: