Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria.
Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC umemalizika tarehe 20 Agosti 2017 katika mji wa Pretoria Afrika Kusini ambapo Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa kauli moja wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika Asasi ya Ushirikiano wa siasa , Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo.
Tanzania imemaliza kipindi chake cha Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 19 Agosti, 2017 wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa SADC ambao umefanyikia hapa Pretoria, Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
Akizungumzia mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema pamoja na mambo mengine SADC imetambua na kuthamini mchango wa Tanzania katika kipindi cha Uongozi wa Asasi ya Saisa , Ulinzi na Usalama iliyokuwa chini ya Rais Dkt. John Pombe magufuli.
Amesema Tanzania imeshakuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo mara tatu, kwa nyakati tofauti ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni kipindi cha 2006/2007 na mara ya pili ilikuwa ni 2012/2013 na mara ya tatu katika kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo alikabidhiwa kijiti cha uongozi huo kutoka kwa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Falme ya Swaziland tarehe 30 Agosti, 2016.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika Asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi wa Bungenchini Seychelles ambao ulifanyika mwezi Septemba, 2016.
Aidha katika kipindi cha Uongozi wa Tanzania ulisaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Lesotho ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa pamoja na kushughulikia matatizo ya Uchaguzi nchini DR Congo.
Mkutano wa 37 wa SADC pia umemuongezea muda mwingine Mtanzania Dkt. Stergomena Taxi kuendelea na wadhifa aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha miaka minne mingine ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2021.
Dkt. Tax amethibitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliomaliza na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) umehitimishwa kwa kutolewa Tamko (Communique) kuelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali ikiwa ni pamoja na mkutano wa 38 kufanyika nchini Namibia
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini
20 Agosti, 2017.
No comments:
Post a Comment