Kimya kikubwa kilitawala mbio za
mita 100 wanaume katika fainali za mabingwa wa dunia katika uwanja wa
London pale Usain Bolt aliposhindwa kutwaa medali ya dhahabu.
Bolt ambaye hizo ni mbio zake za
mwisho kabla ya kustaafu kabisa riadha, alijikutwa akishindwa na
Mmarekani Justin Gatlin.
Shamra shamra za kumshangalia Bolt
zilitumbukia nyongo, baada ya Mmarekani Gatlin ambaye alinaswa mara
mbili kutumia dawa za kututumua misuli kushinda.
Muonekano kwa picha iliyopigwa kutokea juu unavyoonyesha Gatlin akimaliza wa kwanza kabla ya Bolt
Justin Gatlin akipiga magoti kutoa heshima kwa Usain Bolt ambaye atastaafu baada ya michuano hiyo
No comments:
Post a Comment