Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mama Mary Mdachi, mjane wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo ya msiba wa Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Kitivo cha Uhandisi katikla idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment