Wenyeviti 50 wa Serikali za Mitaa wa CUF Mkoa wa Dar es Salaam wametangaza kuunga mkono uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF la upande wa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa vua uanachama wabunge wanne wa viti maalumu na madiwani wawili.
Wabunge waliovuliwa uanachama ni Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally, Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Raisa Abdallah Mussa, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.
Wakiwakilisha wenzao 36 wenyeviti 14 kutoka mitaa mbalimbali ya halmashauri za manispaa tano za Dar es Salaam wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhisha na kazi nzuri inayofanywa na Profesa Lipumba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake 14 mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi amewaambia wanahabari leo Jumanne Agosti 8 wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao wamebainika kukihujumu chama hicho.
"Tunamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF," amesema Shilingi
Mbali na hilo Shilingi amewataka watu wanaoingilia mgogoro wa chama hicho kuacha mara moja na kwamba mgogoro ni wa kikatiba na suala hilo lipo mahakamani muda si mrefu uamuzi utatolewa.
No comments:
Post a Comment