Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusina na uzinduzi wa kampeni yao itakayojulikana kwa jina la UZALENDO KWANZA. Pichani kulia ni Msanii wa Filamu Wastara na kulia kwake ni Misayo Ndumbagwe.
kampeni hiyo imezinduliwa rasmi leo, ikiwa na lengo la kuunga mkono jitihada na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo ambapo
wasanii wa muziki na filamu wapatao 250 wameshirkishwa pamoja na wachezaji wa mpira.
wasanii wa muziki na filamu wapatao 250 wameshirkishwa pamoja na wachezaji wa mpira.
Steve
amesema kuwa, ni wakati sasa kwa Watanzania kujenga utamaduni wa
kuvienzi na kuvipenda vitu vyao kwa namna moja ama nyingine katika
nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa sababu nchi ni Yetu,rasimali
zilizopo ni zetu,madini ni yetu,mbuga za wanyama ni vya kwetu, hivyo ni
muhimu Watanzania wakaamka sasa na kuonesha uzalendo wao halisi kama
ambavyo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akionesha kwa vitendo na
kusisitiza suala zima la Uzalendo ndani ya nchi yetu.
"Sisi
kama Wasanii, kwa moyo mmoja tumeamua kushikamana kwa pamoja na baraka
zote tunazo kushikamana na kuiunga mkono kauli mbiu ya Rais Dkt Joh
Pombe Magufuli ya UZALENDO KWANZA kuwa na harakati za kuifanya Tanzania
yetu na Watanzania wenyewe kuwa Wazalendo kwa nchi yao",alisema Steve
Nyerere na kuongeza kuwa kauli mbiu hiyo sio kwa ajili ya Dar Es Salaam
tu bali,ni kwa ajili ya Tanzania nzima.
Mwenyekiti
wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza Steven Mengele almaarufu kwa jina la
kisanii Steven Nyerere akitoa ufafanuzi zaidi kuhusina na kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA mbele ya Waandishi wa habari (hawapo
pichani) mapema leo jijini Dar,kampeni hiyo inatarajia kuhamasishwa mikoa mbalimbali nchini .Pichani kushoto ni Msanii wa
Filamu ni Misayo Ndumbagwe pamoja na Kemmy .
Baadhi
ya Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni
hiyo ya UZALENDO KWANZA,itakayosambazwa nchi nzima kuhakikisha wananchi
wanaelewa dhana nzima ya kuwa mzalendo na nchi yako.
Mkutano ukiendelea mapema leo wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Msanii
wa Filamu Wastara Juma akiwahimiza Watanzania kuwa WAZALENDO KWANZA
katika mambo mbalimbali ikiwemo kuvithamini vya vyumbani,pia amewaomba
Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wao kwa kununu kazi zao zilizo halisi
na halali ili kuhakikisha dhama nzima ya UZALENDO KWANZA inatimia.
Baadhi
ya Wasanii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya UZALENDO KWANZA,itakayopita mikoa mbalimbali kuwahamasisha
wananchi kuwa Wazalendo na nchi yao na pia kumuunga mkono Rais Dkt John
Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele
kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment