KLABU ya Simba huenda ikaachana na Kocha wake wa Sasa Mcameron Joseph Omog, Taarifa ambazo siyo Rasmi (Ambazo Simba wenyewe hawajathibitisha wazi) ila zinatoka kwa baadhi ya watu wa ndani kabisa wa klabu hiyo ni kwamba Simba imempa sharti moja tu kocha wake sharti lenyewe akitakiwa kushinda mechi 5 zinazofuata endapo atashindwa kufanya hivyo basi atafungashiwa virago.
Omog amekuwa akilaumiwa na baadhi ya washabiki na wanachama kuwa mzito kufanya mabadiliko (Substitutions) Kiasi kwamba wanapoingia wachezaji ambao walalamikaji wamekuwa wakiamini wanaweza kuwapa matokeo mapema inakuwa haina madhara kwa Timu pinzani.
Kocha OMOG katika mechi mbili za mwanzo za Ligi kuu Bara VPL ameshinda mechi moja dhidi ya Ruvu Shooting akishinda bao 7 kwa 0 kabla ya Kuja kutoa sare ya bila Kufungana na Azam Fc Simba ikicheza kwa mara ya kwanza na Azam katika uwanja wa Azam (Azam Complex)
No comments:
Post a Comment