Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda(Uganda Cranes) na Klabu ya Simba Emmanuel Okwi ameshinda Tuzo kama mwanamichezo bora wa Mwezi wa 8 huko nchini Uganda, Tuzo ambayo huwa inaandaliwa na Eastern Uganda Sports Press Assosiation (EUSPA)
Moja kati ya sifa kubwa iliyomfanya OKWI kupata tuzo hiyo msomaji wa Kwataunit Blog ni goli pekee alilofunga dhidi ya Misri, Goli ambalo liliwawezesha Uganda kushinda dhidi ya wababe hao wa Soka la Afrika baada ya miaka 52 .Okwi amepata jumla ya Kura 300 ambazo ndizo zimemfanya kushinda Tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment