Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus (kulia) wakati Rais huyo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus akiwasilisha taarifa ya wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao cha wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu mara baada kufungua kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa
viwanda vya mazao ya misitu nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale
inapohitajika kwa kuzishughulikia
changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya
awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.
Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kutatua
changamoto zinazowakabili ili
kuwawezesha wamiliki wa viwanda hivyo
hasa wazawa kutoa ajira nyingi kwa wananchi.
Amesema
Wizara hiyo haiwezi kufanya kazi pekee
yake pasipo kushirikiana na sekta binafsi kwani wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira
kwa wananchi ambao ndio walinzi wakubwa misitu nchini.
Akizungumza
kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) na Wawakilishi wa
Wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu nchini,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwataka wadau hao wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na
jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao
‘’Nimechaguliwa
na Mhe. Rais kuja katika Wizara hii kwa ajili ya kufanya kazi nanyi, tufanye
kazi kwa ushirikiano’’ alisema Hasunga
Aidha,
Naibu Waziri huyo, amelisema Serikali imeanzisha utaratibu wa ugawaji wa vitalu kwa njia
mnada na kwa njia ya makubaliano
binafsi lengo lake sio kuviua viwanda wa mazao ya misitu vya vinavyomilikiwa wazawa bali
ni kutaka kila mwenye sifa asiweze kukosa mgao huo.
Akifafanua
kuhusiana na utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu ulioanza mwaka jana ,
Hasunga alisema asilimi 30 ya vitalu imekuwa ikifanyika kwa njia ya mnada na asilimi 70 imekuwa
ikifanyika kwa njia ya makubaliano binafsi hali iliyopelekea kupunguza
malalamiko na pamoja na vitendo vya rushwa kwa wadau.
‘’Kila
mmoja wetu hapa atakuwa shahidi hakuna hata mmoja mwenye kiwanda cha mazao ya
misitu aliyekosa mgao kupitia huu utaratibu mpya ulianza kutumika mwaka
jana’’
Alisema
kuwa licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu juu ya
utaratibu huo mpya ambao wengi ni wazawa
kwa kushindwa kushindana na matajiri
lakini hata hivyo utaratibu huo kwa njia
ya mnada umeisaidia serikali k kupanga bei stahiki ya soko katika njia ya makubaliano
binafsi.
Hasunga
alisema Serikali ipo tayari kupokea mawazo mapya kutoka kwa wamiliki wa viwanda
hivyo kama wataona kuna umuhimu wa kuboresha utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu.
Wakati
akijibu hoja za wadau hao, Hasunga aliwaagiza waandae ripoti itayoonesha changamoto
zinazowakabili na kuiwasilisha ofisini kwake ifikapo tarehe 10 mwezi ujao kwa ajili ya
kufanyiwa kazi
Pia, Aliwaagiza wamiliki wa viwandao hao
kuunda kitengo kitakachokuwa na jukumu la kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo kujua masoko pamoja na teknolojia rafiki ya kuzalisha bidhaa zao zitakanazo na mazao ya misitu
Awali,
Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus wakati
akiwasilisha taarifa yake ameiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia wamiliki wazawa viwanda
vya mazao ya misitu kwa vile viwanda vilivyo vingi vimeshindwa kujiendesha
kutokana na kukosa malighafi kwa kuwa wazao hao wameshindwa kushindana na matajiri wakubwa
wakati vitalu vinapouzwa kwa njia ya mnada.
Aliongeza
kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) iangalie uwezekano wa kupunguza bei za
vitalu hivyo kwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kwa vile bei ya
soko la mbao limeporomoka kutokana na watu
binafsi kuuza mbao kwa bei nafuu zilizotokana na miti iliyovunwa ikiwa michanga.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha
Umoja wa Wavunaji Sao Hill, Christian Ahiya, ameiomba Wizara kuona
uwezekano wa kupunguza tozo 32 zinazotozwa
kwa wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu kwa upande wa wilaya Mufundi
kwa kuwa hali hiyo imekuwa ukiwaumiza na
kuwadidimiza.
No comments:
Post a Comment