Mmoja wa wanufaika wa USD 5,000 kutoka Tony Elemelu Foundation akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Jagrin Agriculture Co. Ltd, Riziki Messa akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Habari wa UBA Tanzania, Ms Brendansia Kileo akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Mkutano huo ukiendelea na wanahabari.
Washiriki katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo.
Watanzania wamehamsishwa kujitokeza kwa wingi katika kutumia fursa ya kupewa mitaji kwaajili ya wajasiliamali ambayo inatolewa na taasisi ya Tony Elemelu Foundation.
Katika Semina iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana Mkuu wa idara ya Masoko na Habari wa UBA Tanzania, Ms Brendansia Kileo amesema kuwa kwa sasa maombi bado yanaendelea na wale wote wenye wazo la biashara wanaweza kushiriki kwa mujibu wa waelekezo.
Aliwataka wenye wazo na ndoto za biashara kuzitimiza kwa kuomba nafasi ya kupewa mtaji kupitia asasi ya 'Tony Elemelu Foundation' ambayo watakaofanikiwa kupata watapewa USD 5,000 ikiwa ni mtaji wa mawazo ya biashara yao.
Alisema maombi kuhusiana na kuomba na kupata mtaji yanafanyika kupitia tovuti ya Tony Elemelu Foundation http://www.tonyelemelufoundation.org.
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa USD 5,000 kutoka Tony Elemelu Foundation walioshinda kutokea Tanzania katika miaka ya nyuma wamewataka idadi kubwa ya Watanzania kushiriki katika fursa hiyo ili waweze kufikia malengo yao.
Akizungumza mmoja wa wanufaika Mkurugenzi wa Jagrin Agriculture Co. Ltd, Riziki Messa alisema yeye pamoja na wenzake waliowahi kunufaika na fursa hiyo ya ujasiliamali amesema wamedhamiria kuhamasisha Watanzania wengi kushiriki katika fursa hiyo kutoka taasisi ya Tony Elemelu Foundation.
Aliwataka wanahabari kutumia fursa hii kwa ajili ya kuutangazia umma wa Watanzania kuomba kwa wingi ili kusudi Tanzania iweze kuwa na vijana wengi watakaonufaika na programu hii ya kutoa mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara au kuanzisha biashara.
No comments:
Post a Comment