- Maumivu
ya tumbo chini ya kitovu husumbua wasichana na wanawake wengi wakati wa
hedhi zao. Maumivu haya yanaweza kuwa kidogo au wakati mwingine kuwa
makali sana kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya shughuli nyingine.
Maumivu ya Tumbo Yanavyotokea
Maumivu haya
hutoka kwenye tumbo la uzazi. Wakati wa hedhi ukuta wa mji wa mimba
huanza kubomoka na kisha kusababisha damu kutoka. Wakati ukibomoka
misuli ya tumbo la uzazi hukaza na kusinyaa, kukaza huku ndiko
kunakosababisha maumivu wakati wa hedhi.
Licha ya
maumivu haya kusababishwa na kukaza kwa tumbo la uzazi, kuna magonjwa
mengine yanaweza kuchangia kuleta hali hii. Mara nyingi maumivu ya namna
hii huwa makali zaidi kiasi cha kumfanya mtu ashindwe kuendelea na
shughuli zake. Hali kama;
- Endometriosis (uwepo wa tishu za ukuta wa mji wa mimba sehemu nyingine kama kwenye ovari au misuli ya mji wa mimba)
- PID (Maambukizi kwenye via vya ndani vya uzazi)
huweza kuchangia kuleta hali hii.
Matibabu
Matibabau ya
hali hii inategemea na kiasi cha maumivu. Kama maumivu ni kidogo,
yanaweza kuvumiliwa na baada ya hedhi kuisha. Njia nyingine za kupunguza
maumivu wakati wa hedhi;
- Kukanda tumbo kwa maji ya moto
- Kunywa kinywaji chenye moto
- Usinywe vinywaji vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa
- Tumia dawa MEFENAMIC ACID vidonge kupunguza maumivu badala ya kutumia dawa za maumivu kama diclofenac na diclopar
Unapoona unapata maumivu makali sana ni vizuri uonane na mtaalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Chanz0: Doctorjoh Blog
Chanz0: Doctorjoh Blog
No comments:
Post a Comment