Baada ya kujifungua akina mama wengi huendelea kunyonyesha mpaka miaka
miwili, japokua wengine hunyonyesha chini ya hapo inategemea na mtazamo
wa mtu. lakini kitaalamu mtoto anayenyonya kwa miaka miwili hua anakua
vizuri na kua na uwezo sana wa kiakili..kipindi cha kunyonyesha mama
anaweza kuugua au kutumia dawa fulani fulani kwa ajili yake. baadhi ya
dawa hazitakiwi kutumika kwa mama kipindi hichi kwani zinaweza
kumuathiri sana mtoto na kuharibu ukuaji wake..hebu tuzione dawa hizo.
Chloramphenicol; hii ni antibayotiki, ni dawa inayotumika kuua
bacteria ambao wanashambulia mwili. kwa hapa tanzania dawa hii mara
nyingi hutumika kutibu ugonjwa wa typhodi.dawa hii husababisha ugonjwa
unaitwa grays syndrome yaani mtoto hubadilika rangi na kua rangi ya gray
lakini pia huonyesha dalili kama kutapika, tumbo kuvimba, kukosa hamu
ya kula, kushuka kwa joto na presha kushuka.lakini pia dawa hii huzuia
utengenezaji wa damu kutoka kwenye mifupa[aplastic anaemia].tatizo hili
la damu likishaanza hakuna dawa inayoweza kumponya mtoto huyu.
Dawa ya mseto ya malaria; dawa hii hutumika kutibu malaria lakini
hua inapita kwenye maziwa na kuingia kwa mtoto. kama una mtoto mwenye
chini ya kilo tano usimeze dawa hii kwani ikiingia kwa mtoto hawezi
kuitoa nje lakini kama mtoto wako ana zaidi ya kilo tano unaweza
kutumia.
Vidonge vya uzazi wa mpango; hizi ni dawa ambazo hua zina homoni
za oestrogen na progesterone matumizi yake husababisha kiwangi kikubwa
sana cha homoni hizi mwilini na kuzuia mimba. lakini dawa hizi hupingana
na homoni ya prolactin ambayo ni muhimu kwa kutoa maziwa.hivyo matumizi
ya dawa hizi kwa mama mwenye mtoto chini ya miezi sita hupunguza maziwa
kwa kiasi kikubwa.
Aspirin; aspirin ni dawa ya maumivu lakini pia hulainisha damu na
kuifanya kua nyepesi sana hii ni hatari kwa mtoto kwani anaweza kuvuja
damu mpaka kufa lakini pia husabibisha ugonjwa unaitwa reyes syndrome
ambao huambatana na kuvimba maini na kichwa.
Dawa za cancer; kuna dawa aina mbali mbali za kansa ambazo mara
nyingi huu seli za kansa au kuzuia zisikue.kwa jinsi zinavyofanya kazi
hupunguza kinga ya mwili ya mgonjwa pia hupita kwenye maziwa ya mama na
kushusha kinga ya mtoto na kumfanya aharishe.
Ergotamine; hii ni dawa inayotumika kutibu maumivu makali ya
kichwa kitaalamu kama migraine headache, mara nyingi huchangwanya na
kemikali ya caffeine kufanya kazi vizuri. matumizi yake hupunguza
utengenezaji wa maziwa ya mama na huweza kuleta degedege kwa mtoto.
Adrogens; hizi ni hormone ambazo zinapatikana kwenye mwili wa
binadamu lakini pia zinatengenezwa kiwandani kutolewa kwa watu ambao
wana upungufu wa homoni hizi.kwenye mwili wa mwanamke homoni hizi
hubadilika na kuwa oestrogen yaani homoni ya uzazi.sasa matumizi ya dawa
hizi hupunguza kiasi cha maziwa kwa mama.
Metformin; hizi ni dawa za kisukari, hupewa kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari lakini dawa hizi zina uwezo wa
kupita kwenye maziwa na kushusha sukari kwa mtoto..hii ni hatari sana na
huweza kuua.
Lithium; hii ni dawa inayotumika kwa wagonjwa wa akili, mama
ambaye pia ana ugonjwa wa akili anaweza kupata mimba pia au mama
aliyekua mzima anaweza kupata ugonjwa wa akili baada ya kuzaa. dawa hii
hubadilisha mapigo ya moyo ya mtoto na kuyapeleka tofauti.
Iodine; hupewa kwa watu wenye kiwango kidogo sana cha iodine
mwilini lakini pia inapatikana kwenye chumvi.matumizi makubwa ya iodine
husababisha kuvimba kwa goita na kiwango kidogo cha homoni za thyroid
kwenye mwili wa binadamu.
Mwisho; kuna dawa nyingine nyingi huenda sijazitaja hapo lakini
hizo ni baadhi ambazo zinapatikana kwa wingi. katika kipindi hicho cha
unyonyeshaji basi ni vizuri kuongea na doctor kabla ya kumeza dawa
yeyote.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
-
No comments:
Post a Comment