Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii, Nape Nnauye amesema anatamani bunge lisiwe la kutunga sheria tu bali pia lifute sheria za hovyo au kuzirekebisha.
Pia Nape ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya uchambuzi wa sheria zake na kuangalia namna ya kuondoa sheria kandamizi katika sekta ya utalii ili taifa linufaike na rasilimali zilizopo katika sekta hiyo.
Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo Mjini Dodoma leo Jumatano Machi 28, Nape amesema zipo sheria ambazo ni kandamizi hivyo wizara inapaswa kuzichambua na kupeleka bungeni ili ziondolewe au zifanyiwe marekebisho.
“Fanyeni uchambuzi wa sheria kandamizi, mi natamani bunge lisiwe la kutunga Sheria tu ,bali pia lifute Sheria za hovyo au kuzirekebisha,” amesema Nape.
Aidha, ameitaka wizara hiyo kuongeza vigezo vya kupima madhara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sekta ya utalii lakini pia kutoa taarifa ya uchambuzi wa kodi mbali mbali katika wizara hiyo.
“Naomba tusijpe muda mrefu wa kupima madhara ya VAT, wenzetu Kenya wameshafuta hiyo, sasa hadi wamefuta wao si wajinga,” ameeleza.
No comments:
Post a Comment