Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wa mataifa yote na wa
umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa
kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata
chunusi. Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga
wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla
tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa
binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana
na chunusi.
Katika mwili wa binadamu, chunusi huonekana zaidi maeneo ya usoni,
mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni. Kutegemeana na uwingi wa
chunusi hizo, mwathirika huweza kunyanyasika kimawazo na kupata makovu
juu ya ngozi yake. Kuna dawa za kutibu chunusi ingawa ni ugonjwa
unaoweza kujirudiarudia. Chunusi huondoka polepole sana na wakati
mwingine chunusi mpya huanza kujitokeza kabla nyingine kupona kabisa. Ni
ugonjwa unaotakiwa kupewa tiba ya mapema ili kuepuka kupata madhara ya
kudumu.
Chanzo Cha Chunusi Ni Nini?
Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha
mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu
vya vinyweleo (hair follicles). Picha hapa chini inaonyesha muundo wa
kitengo kimoja cha kinyweleo (pilosebaceous unit).
Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi
ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi
vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya
mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. vitengo
hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.
Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.
Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa
kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali
inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa
miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.
Sebum hii iliyotengenezwa na sebacious gland huchanganyikana na seli
za ngozi zilizokufa na kwa pamoja hutolewa nje ya mwili kupiti vijitundu
vya vinyweleo. Vijindu hivi vikijaa mchanganyiko huo, humwaga ziada juu
ya ngozi na na kuifanya kuwa laini. Hali hii ikiendelea bila dosari,
ngozo hubaki laini na yenye afya.
Chunusi za aina mbalimbali hutokea pale kunapotokea dosari katika
ufanyaji kazi wa vijitengo hivi vya kwenye ngozi. Tutaelezea dosari
mabilimbali zinazoweza kutokea, na nini kitaonekana juu ya ngozi ya mtu
huyu. Kuna dosari ambazo zitaleta vijipele vya kawaida na nyingine
kuleta mapele makubwa, mara nyingine yaliyotunga usaha.
Kuna hali mbalimbal ambazo zinaweza kutokea kwa chunusi kwenye ngozi. Kwa kawaida chunusi huanza kwa sababu zifuatazo:
. Seli za ngozi zilizokufa (corneocytes) hugeuka na kuwa nzito na katika kutembea kwenye kijitundu cha kinyweleo
huganda badala ya kutoka nje ya tundu
. Seli nyingi za ngozi kutokea sehemu ya juu ya tundu kuliko sehemu ya chini ya tundu la kinyweleo
. Uzalishaji wa mafuta (sebum) kuongezeka
Kuongezeka kwa vitu hivi ndani ya kijitundu cha kinyweleo, huziba
sehemu ya juu ya kijitundu na kuzuia vitu hivi visitoke nje, hali ambayo
kiutaalamu huitwa microcomedone. Bakteria waitwao Propionibacterium
acnes, huishi ndani ya vijitundu hivi vya vinyweleo na hutumia sebum
kama chakula chao. Kuongezeka kwa sebum hufanya bacteria hawa kuongezeka
ndani ya vijitundu hivi lakini hawaleti madhara yo yote kwa sababu hadi
sasa wanaishi ndani ya vijitundu tu – hawana madhara kwenye ngozi.
Whitehead – Closed Comedone
Kuongezeka kwa sebum na seli zilizokufa kutajaza vijitundu vya
vinyweleo na kuufanya mchanganyiko huu kuwa mzito. Endapo vijitundu
vitakuwa vidogo au vimeziba hali inayoitywa closed comedone au whitehead
itajitokeza.
Kuendelea kujazana kwa mafuta kutasababisha eneo linalozunguka
kijitundu hicho kuvimba. Whiteheads huweza mara nyingine kuambatana na
mashambulizi ya bacteria – P.acnes bacteria – kutegemeana na kama
bakteria hao waliweza kushambulia seli zinazolizunguka tundu.
Blackhead – Open Comedone
Kama katika kuongezeka huku kwa sebum na seli za ngozi zilizokufa,
kijitundu cha kinyeweleo kitakuwa wazi, hali inayoitwa open comedone au
blackhead itatokea.
Kuzidi kuongezeka kwa mafuta kutoka sebacious glands, kutalifanya
eneo linalokizunguka kijitundu cha kinyweleo kuvimba. Blackheads
zinaweza kuambatana na mashambulizi ya bakteria wa P.acnes endapo
wataweza kushambulia eneo linalozunguka kijitundu cha kinyweleo.
Chunusi – Pimple
Kuzidi kuongeka kwa sebum kutoka kwenye sebacious glands na seli
zilizokufa kutajenga msukumo kwenye seli zinazokizunguka kijitundu cha
kinyweleo. Msukumo ukiwa mkubwa wa kutosha, kuta za kijitundu hupasuka
na mafuta kupenya kwenye ngozi ya karibu. Kwa sababu mafuta haya yana
uwingi wa bakteria wa P.acnes, ngozi hii inayozunguka kijitundu
hushambuliwa na bakteria hawa na kuifanya ngozi hiyo kuwa na uvimbe
nwekundu (pimples). Hali hii
kiutaalamu huitwa inflammatory papule.
Chunusi – Pustule
Chunusi za aina ya pustule hutofautiana na pimples au papules kwa kuwa
na chembechembe nyeupe za damu (usaha). Wakati mwili unapambana na
bakteria wa P.acnes, chembechembe nyeupe za damu ambazo ni sehemu ya
kinga za mwili, hujazana na kutunga usaha katika vijitundu vya
vinyweleo. Kwa sababu ambazo bado hazijafahamika vizuri kisayansi,
chunusi nyingine hutunga usaha wakati nyingine hazitungi.
Chunusi – Cyst (Nodule)
Wakati mwingine mafuta na bakteria wanaposambaa kwenye ngozi
inayozunguka kijitundu, maambukizi husambaa eneo kubwa na huelekea chini
zaidi ndani ya ngozi na kusababisha vijinundu (nodules or cysts) na
makovu. Vijinundu hivi huleta maumivu makali na haviponi kwa urahisi.
Mambo Gani Huongeza Uwezekanao Wa Kuwa Na Chunusi?
Chunusi ni kitu cha kurithi, endapo wazazi wako walikuwa na chunusi
basi uwezekano wa wewe kuwa na chunusi ni mkubwa sana. Chunusi pia
hushambulia watu wakiwa katika umri wa barehe na ujanani wakati homoni
kama za testosterone zinaongezeka mwilini. Wanawake hupata chunusi zaidi
wanapofikia umri wa kuanza kupata siku za mwezi. Wanawake wengi huota
chunusi siku chache kabla ya kuingia mwezini.
Kuna vitu vinavyoweza kuchangia kupata chunusi:
. Kuvaa vitu vinavyobana, vinavyosugua juu ya ngozi, kama, helmets, mikanda ya sidiria, sweta za kukaba shingo n.k.
. matumizi ya vipodozi vya ngozi au nywele vyenye vitu vibaya
. Kuosha uso mara nyingi au kuusugua uso kwa nguvu. Matumizi ya
sabuni zisizofaa au maji ya moto sana huongeza makali ya chunusi.
. Kuwa na msongo wa mawazo mara kwa mara.
. Kugusa uso mara kwa mara.
. Kuvuja jasho.
. Kuacha nywele zining’inie juu ya uso na kuufanya uso kuwa na mafuta zaidi.
. matumizi ya baadhi ya madawa.
. Kufanya kazi kwenye mazingira ya mafuta au kemikali kwa muda mrefu.
Tiba Ya Chunusi
Tiba ya chunusi itazingatia zaidi aina ya chunusi iliyotokea. Lakini kwa ujumla tiba hizo zinalenga kufanya yafuatayo:
. Kupunguza kunata kwa seli za ngozi zilizokufa ili ziliweze
kutiririka kiurahisi na kutoka nje ya vijitundu vya kwenye ngozi. Lotion
kama salicylic acid 2% zinaweza kutumika.
. Kuua bakteria wa P.acnes kwa kutumia antibiotics za aina mbalimbali, kwa mfano, benzoyl peroxide.
Pia dawa nyingine kama Tretnoin cream ni nzuri kwa tatizo la chunusi
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment