HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » JINSI YA KUTAMBUA KAMA UNA UZITO MKUBWA KUPINDUKIA

Uwiano wa uzito wa mwili kulingana na urefu wa mtu hujulikana kitaalam kama body mass index(BMI). Uwiano huu hupatikana kwa njia ya hisabati ambapo hugawanywa uzito wa mwili katika kilogramu (kg) kwa Kipeo cha pili cha urefu wa mwili katika mita (m)². Kwa hiyo kanuni huwa kama ifuatavyo:

BMI=              Uzito wa mwili katika kilogramu                  =  kg
           Kipeo cha pili cha urefu wa mwili katika mita             (m)².

BMI hutusaidia kuweza kujua kama mtu ana uzito mkubwa, uzito wa kawaida au uzito mdogo. Walio na uzito mdogo ni wale walio na BMI chini ya 18.5, na uzito wa kawaida ni BMI kati ya 18.5 hadi 25 na wale walio na BMI ya 25 na kuendelea ni wenye uzito mkubwa (overweight), BMI zaidi ya 30 ni uzito uliopindukia (Obese).
Mfano: 
Edna (jina sio halisi) ni msichana mwenye umri wa miaka 26 na ana uzito wa kilogramu 85.Urefu wake ni kimo cha sentimita 169. Je BMI yake ni ngapi?
Jibu:
Edna ana BMI ya 29.76 kg/(m)²  (angalia jedwali jinsi ya kukokotoa).
Je Edna atahitajika kuongeza au kupunguza uzito wa mwili?
Jedwali la kukokotoa
KANUNI YA BMI
 BMI=              Uzito wa mwili katika kilogramu                  =  kg
              Kipeo cha pili cha urefu wa mwili katika mita          (m)².
KUBADILI SENTIMITA KUWA MITA (mita 1= sentimita 100)
169 ÷ 100= 1.69m,      kwa hiyo urefu wa Edna ni sawa na kimo cha mita 1.69.
KUKOKOTOA BMI
BMI=         85kg                  = 29.76 kg/(m)² . 
            (1.69m x 1.69m)
Kama una uzito mkubwa au uzito wa kupindukia, kupunguza uzito ni njia thabiti ya kuweza kukuepusha na magonjwa hatari yatokanayao na kuwa na uzito mkubwa au uzito mkubwa kupindukia. Magonjwa hatari tunayoweza kupata kutokana na kuwa na uzito mkubwa ni kama yafuatayo:
  • Magonjwa ya moyo.
  • Shinikizo kubwa la damu.
  • Kiharusi.
  • Aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari.
  • Baadhi ya aina za saratani.
  • Ugumba.
  • Msongo wa mawazo.
  • Ugonjwa wa mifupa na
  • Maumivu ya mgongo.

IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: