
Kukojoa
damu ni dalili ya kuonyesha kuwa mtu anayekojoa ana magonjwa katika
mfumo wa mkojo kama vile magonjwa ya kichocho au magonjwa mengine
yanayoshambulia kibofu cha mkojo au kwenye figo.
SABABU
Magonjwa
yanayoshambulia mfumo wa mkojo kama vile UTI, magonjwa ya zinaa hasa
kwa wanawake, vijidudu kama staphylococcus saprophyticus, mawe kwenye
figo (kidney stone) kuvimba kwa tezi zinazozalisha manii kwa wanaume
ambao umri umeenda yaani wazee.
Sababu nyingine ni kama kupata ajali na kuumia sehemu za mfumo wa mkojo
(trauma), kupata magonjwa kama kansa ya kibofu cha mkojo, hii hutokea
mara nyingi hasa vijijini ambapo watu wanacheza au kuogelea kwenye
madimbwi ya maji yasiyotembea.
Sababu zingine ni mtu kuugua magonjwa ya sickle cell anemia na magonjwa
mengine ya figo kama vile nephotic syndrome na mengine mengi ambayo
yanajulikana kwa kitaalamu na siyo rahisi kuyafafanua kwa Kiswahili.
AINA YA UGONJWA WA KUKOJOA DAMU
Kuna
aina mbili za damu kutoka kwenye mkojo, moja ni ile ambayo damu
huchuruzika na kuonekana vizuri kwenye mkojo. Hii hujulikana kama
macroscopic haematuria au gross haematuria ambayo hutokea kwa wagonjwa
wa kichocho au waliopata ajali.
Nyingine ni ile inayoonekana kwa
mbali na mara nyingine huonekana wakati mgonjwa anapopimwa mkojo, aina
hii hujulikana kama microscopic haematuria.
JINSI YA KUGUNDUA TATIZO (diagnosis)
Mara
nyingi tatizo la kukojoa damu hugundulika baada ya mgonjwa kwenda
hospitalini na kuonana na daktari na akachukua maelezo yake vizuri na
kuagiza mgonjwa akapime mkojo.
Kipimo cha Ultrasound pia husaidia kujua tatizo linalosababisha mgonjwa akojoe damu.
Mashine
ya X- ray husaidia kugundua kama mgonjwa ana mawe kwenye figo. Kipimo
kingine cha kisasa ni CT scan hiki kina uhakika ila ni ghali sana na
hupatikana kwenye hospitali kubwa.
TIBA
Tiba
ya uhakika ni kujua sababu inayosababisha mgonjwa akojoe damu kama ni
kichocho basi mgonjwa atapewa dawa ya kichocho na kama ni UTI mgonjwa
atapewa dawa husika na kama ni magonjwa ya zinaa nayo yatatibiwa.
Magonjwa mengine ni kama yale ya figo basi nayo yakigundulika
yatatibiwa.
USHAURI
Watoto
wasichezee maji yaliyosimama hasa kwenye mabwawa vijijini na mijini,
wakigundulika kuwa walicheza basi haraka wapelekwe hospitali kupimwa.
No comments:
Post a Comment