Wakati wa kuzaliwa; mtoto hupungua uzito kwa 5% mpaka 10% ndani ya siku saba mpaka kumi za kuzaliwa, baadae mtoto huongezeka kilo mbili kila mwaka mpaka atakapofikisha miaka mitano, mtoto huzaliwa na urefu wa sentimita 50, baada ya mwaka mmoja hufikisha sentimita 75 na na baada ya miaka minne hufikisha urefu wa sentimita 100.
mtoto huzaliwa na kichwa chenye mzunguko au diameter au mzunguko wa sentimita 35 na kuongezeka sentimita moja kila mwezi na baada ya miezi 12 kichwa hufikisha sentimita 46
Wiki ya sita; katika umri huu mtoto huanza kutabasamu bila kuongea chochote.
Mwezi wa pili; mtoto huanza kukunja na kunyoosha mikono huku akivuta nguo zake na za mtu anayembeba.
Mwezi wa nne; kipindi hiki mtoto huanza kushika vitu na kuviweka mdomoni na kuanza kugeuka pale anaposikia sauti ya mtu inaita na kuweza kutumia shingo lake japokua wakati mwingine huweza kushika shingo akiwa na miezi mitatu tu.
Mwezi wa sita; kipindi hiki mtoto huota meno, huanza kutambaa, huanza kukaa mwenyewe na hupata wasiwasi akimuona mtu ambaye hamfahamu.
Mwezi wa tisa; mtoto huanza kusimama, kuita majina kama dada, mama, kaka na kuanza kucheza michezo ya kitoto.
Mwezi wa 12; mtoto huanza kutembea kwa sapoti ya kushikwa au kutumia vifaa maalumu vya kusukuma, huanza kuongeza maneno zaidi ya kaka na dada na pia huweza kushika kikombe na kunywa mwenyewe.
Mwezi wa 15; mtoto huanza kutembea mwenyewe, huweza kuchora mstari na kuonyesha kitu anachokihitaji kwa kidole.
Mwezi wa 18; mtoto huweza kupanda ngazi, huongeza idadi ya maneno na hufuata akiagizwa kufanya au kutofanya kitu fulani, hapa huanza kutumia kijiko na kujishika sehemu za mwili wake.
Miaka miwili; hapa mtoto huweza kukimbia na kupiga mpira, huweza kuvua nguo na kuanza kutamka maneno kama mimi, wewe yule na kadhalika.
Miaka mitatu; hapa mtoto anazidi kua mkubwa na kuanza kusimama kwa mguu mmoja, kukimbia zaidi, kujua jinsia na umri wake, huweza kuvaa na kuvua nguo lakini hawezi kufunga vifungo, anaweza kuhesabu moja mpaka kumi kama akifundishwa, anaweza kuruka na kuchora duara.
Miaka minne; mtoto anaweza kusimulia kitu kilichomtokea, kutumia choo na kufunga vifungo, huweza kucheza michezo mingi zaidi, huweza kuruka kwa mguu moja bila kuanguka.
Miaka mitano; mtoto anaweza kuzitambua rangi nne za msingi, anaweza kuendesha baiskeli, anaongea kama watu wengine bila kuchanganya wakati uliopo na ujao.
Mwisho; utaratibu wa kwenda kliniki kwa muda wa miaka mitano uliwekwa ili kuhakikisha mtoto anafuatiliwa na hachelewi kukua na kama kuna tatizo lolote basi lifanyiwe kazi kwa wakati hivyo ni muhimu kuendelea kwenda kliniki hata kama unaona mtoto amekua.
hatua hizo za ukuaji zinatofautiana kulingana na mataifa mbalimbali lakini mtoto wako akiwahi kufanya vitu sio dhambi ila ukiona anachelewa kupita kiasi basi ni dalili mbaya ya ukuaji na kliniki watakwambia.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment