Nini maana ya presha ya kushuka ?
Hypotension ndio jina linalotumika
kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijawa
wazi.Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine
huwa chini.Hivyo basi namba ya juu kikawaida kwa mtu mzima inapaswa kuwa 100
hadi 139 na ya chini inapaswa kuwa 60 hadi 90.Hivyo bas pressure yako ikiwa
chini ya 100/60 Ndio inajulikana kama Hyptension yaani pressure iko chini.
Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na
kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya
mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni
dalili ya uzima kwao.
Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye
presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya
kiafya huonekana pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa
matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe
na kizunguzungu au kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa. Kushuka ghafla kwa
presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu
aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana kama
postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic
hypotension.
Postural hypotension inachukuliwa ni
hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini
kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na
kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile mapigo
ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo. Kwa
kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya
chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako,
hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya
nini ?
Mwili wako unapeleka taarifa
kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na
kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile.
Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako
itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla.
Kwa ufupi athari ya maradhi ya
presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa
na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jengine la kufahamu
ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri
unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri
unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.
Ni kiwango gani cha presha kinapofika ndio huwa maradhi ?
Hakuna kiwango maalum kinachojulikana ambacho ni sawasawa kwa watu wote
kikifika ndio kinaitwa maradhi. Kiwango ambacho kwako ndio uzima, basi huenda
kwa mwenzako ikawa ni maradhi. Katika presha ya kushuka, madaktari wengi
huchukulia kuwa tayari mtu ana maradhi pale
aambapo kiwango chake cha presha kinafuatana na dali za maradhi yenyewe.
Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachukulia tayari mtu ana maradhi ya presha
ya kushika pale vipimo vinapoonyesha kiwango hichi 90/60 mm Hg. Tufahamu kuwa
kiwango cha namba inayosomwa chini katika kipimo cha presha (… /60 mm Hg ),
hichi huonyesha tayari mtu huyu anapresha ya
chini hata kama kile cha juu ( 90/…mm Hg) kina namba iliyozidi 100. Mfano ikiwa
umepimwa presha na ukapata kipimo hichi 115/60 mm Hg, presha yako itakuwa ipo
chini. Na kama umepata kipimo hichi 115/50 mm Hg, sio kwamba presha yako
itakuwa ipo chini tu, bali presha hii itakuwa si ya kawaida.
Dalili za maradhi
Kama nilivyokwisha tangulia kusema, presha inaweza kuwa sawa kati ya watu
wawili lakini ikawa na matokeo tofauti. Presha hiyo inayoweza kuwa sawa na
ikawa na matokeo tofauti si yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg. Presha yenye
kipimo hichi 120/80 mm Hg, ndiyo nzuri na watu wenye presha hii wanakuwa na
afya nzuri. Kitu muhimu ni kujua, mabadiliko gani yanaleta tatizo katika presha
hata inapelekea kuwa si ya kawaida.
Presha nyingi za watu wanapopimwa huwa zinakuwa kati ya 90/60 mm Hg
(presha iliyo chini) mpaka 130/80 mm Hg (presha iliyo juu). Mabadiliko ya
kushuka presha upande wa chini, hata kama kidogo kiasi cha 20 mm Hg, hupelekea
matatizo kwa baadhi ya watu ( hasa watu wasiofanya mazoezi kila siku).
Mtu mwenye mazoezi ambae presha yake nzuri
(120/80 mm Hg) akapimwa presha na kupata kipimo hichi, 110/60 mm au 120/70 mm
Hg, mtu huyu hatakuwa na tatizo lolote la presha
Kuna aina tatu za presha ya kushuka :
Ø Orthostatic sambamba na postprandial orthostatic (Orthostatic
hypotension, including postprandial orthostatic hypotension)
Orthostatic, hii ni aina ya kwanza ya presha inayosababishwa na kubadili
mazingira uliyonayo kwa ghafla, maranyingi hutokea kwa mtu anayesimama kutoka
alipolala. Presha hii haidumu muda mrefu, kiasi cha sekunde chache mpaka dakika
moja. Ikiwa presha hii itatokezea
Baada ya kula, basi itakuwa ni hatua ya pili (postprandial
orthostatic) .Hatua hii ya pili huwapata zaidi wazee na wenye
presha ya juu.
Ø Neurally mediated hypotension (NMH)
NMH kama ilivyo kifupisho cha presha aina ya pili, huwapata zaidi vijana na
watoto. Presha hii hutokea pale mtu anaposimama kwa muda mrefu. Maranyingi
huwapata sana watoto.
Aina hii ya pili ya presha ya kushuka maranyingi
husababishwa na hali zifuatazo :
• Utumiaji wa pombe
• Utumiaji wa dawa za kutibu presah ya juu.
• Utumiaji wa dawa za kumtoa fahamu mtu wakati wa kufanyiwa upasuaji
Mambo mengine yanayosababisha presha kushuka ni pamoja na :
• Ugonjwa wa Kusukari
• Mtu kula kitu kinachomdhuru
• Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
• Maradhi ya kuharisha
• Kuzimia
• Maradhi ya moyo
• Maradhi ya kustuka
Ø Severe hypotension hii ni aina ya tatu ya
presha ya kushuka ambayo hutokana na kpoteza damu
Kwa muhtasari, dalili za presha ya
kushuka ni pamoja na :
•
Kuona kizunguzungu/kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa
• Kuzimia
• Kushindwa kuzingatia
• Kushindwa kuona vizuri ghafla
• Kuona baridi,
• Kujihisi kuchoka sana
• Kuvuta pumzi kwa tabu
• Kutapika
• Kuhisi kiu
Hali zinazosababisha kupata presha ya kushuka.
Kinachosababisha
presha ya chini bado hakijatambulika hasa. Chanzo chake hakiko wazi. Hata hivyo
mambo yafuatayo yanaweza kuhusiswa nayo :
• Kuwa na mimba
• Matatizo ya homoni mwilini, maradhi ya kisukari, au upungufu wa sukari
mwilini
• Utumiaji mkubwa wa dawa
• Ulaji wa dawa za presha unaopindukia kiwango (Overdose) kwa mtu mwenye presha
ya juu.
• Maradhi ya moyo
• Maradhi ya figo
Nani anapata presha ya kushuka ghafla ?
Presha ya kushuka ghafla inayompata mtu anapoinuka ghafla, inaweza kumpata mtu
yeyote kwa sababu tofauti zikiwemo,
o kuharisha sana,
o kukosa chakula ( njaa kali) kwa muda mrefu,
o kusimama kwa mapigo ya moyo, au
o kuchoka kupita kiasi.
o Pia inawezekana ikawa ni urithi wa maradhi,
o umri mkubwa,
o matumizi ya dawa,
o utapiamlo na
o mambo mengine kama kupatwa na madhara ya jambo fulani.
Nini
kinaifanya presha inayoshuka iendelee ?
Pia Presha ya kushuka mara nyingi huwapata
watu wanaotumai dawa kwa kutibu presha ya juu (hypertension).
Pia huwapata wajawazito au wagonjwa wa kisukari. Mara nyingi wazee nao hupata
maradhi haya hasa wale walio na presha ya juu wakiwa wanaendelea kutumia dawa
zao za presha.
Baadhi ya maradhi ambayo yanasababisha
presha kushuka kuendelea ni pamoja na
ü ukosefu wa vitamin mwilini,
ü madhara kwenye uti wa mgongo, na
ü kensa hasa kensa ya mapafu.
Wakati
gani wa kuchukua hatua za matibabu
Matibabu huanza na hatua zako wewe
mwenyewe. Wakati utakapojiona presha yako inashuka, kaa chini au lala chali na
unyanyue miguu yako juu. Wakati yanafanyika haya, ufanyike utaratibu wa kuonana
na daktari haraka. Pia ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari yanapoonekana
mambo yafuatayo yamemkuta mtu :
• Maumivu ya kifua
• Kizunguzungu
• Kuzimia
• Homa kali sana
• Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
• Kupumua kwa tabu
Pia afuatwe daktari haraka ikiwa baada ya hayo yaliyotokea, kuongezeka na haya
yafuatayo :
• Mtu anapata matatizo makubwa ya mkojo
• Kushinwa kula au kunywa chochote
• Kuendelea kuharisha au kutapika kwa muda mrefu
Matibabu na Dawa
Presha ya kushuka ambayo haijulikani
chanzo chake wala haileti dalili au inampa mtu kizunguzungu anaposimama, mara
chache inaweza kutafutiwa matibabu. Ikiwa zipo dalili, matibabu yataendana na
chanzo chenyewe na daktari atashughulikia hicho chanzo. ( kuharisha,maradhi ya
moyo, kisukari). Ikiwa presha ya chini imesababishwa na matumizi ya dawa kwa
matibabu, basi matibabu yake huwa kubadili dawa nyengine ua kuacha kutumia dawa
kabisa.
Ikiwa hakuna uhakika wa sababu za presha ya kushuka au hayapatikani matibabu
yaliyo sahihi, matibabu sahihi yatakuwa ni kuifanya presha yako ipande na
kuondoa zile dalili zanazokupata inapokujia.
Kwa kutegemea umri wako, hali yako ya kiafya na aina ya presha uliyonayo, mambo
haya yanaweza kukusaidia :
Ø Kuongeza matumizi ya chumvi. Matumizi ya
chumvi lazima yawe kwa kipimo, kwani chumvi nyingi hupandisha presha. Kabla
hujaanza kuongeza matumizi ya chumvi, ni vizuri uwasiliane na daktari ili akupe
kiwango cha matumizi.
Ø Kunywa maji mengi. Kunywa maji
mengi kunamsaidia kila mtu sio mtu mwenye presha ya chini tu. Tunapozungumzia
maji tunalenga zaidi vinywaji na sio maji peke yake, lakini vinywaji vyenyewe
view ni maji, maji ya matunda maziwa na hata kahawa au chai. Tahadhari
ichukuliwe kwa vinywaji vya viwandani kwani huwaletea matatizo baadhi ya watu.
Ø Kuvaa mavazi yenye kubana. Haya ni mavazi ya mpira ambayo
yanavaliwa sehemu za miguuni. Mavazi haya yanasaidia kufanya damu yako isikae
miguuni na iendelee kwenye mzonguko wake kikawaida.
Ø Matumizi ya dawa. Zipo dawa mbalimbali
ambazo zinatumika kufuatana na hali ya presha uliyonayo.
Matibabu hospitalini.
Presha ya kushuka inayomtokezea mtu mwenye
afya nzuri ambayo haina dalili zozote na haimletei matatizo yeyote,
hatahitajika kutumia dawa.Ikiwa zipo dalili, atahitaji matibabu kutokana na
hizo dalili zilizoonekana.Ikiwa presha ulokuwa nayo inatokana na matumizi ya
dawa, daktari atakubadilishia dawa nyengine au utaacha matumizi ya dawa. Wale
wenye NMH pamoja na matumizi ya dawa, inabidi waache tabia
ya kusimama muda mrefu. Kimtazamo presha ya chini inatibika hata kufikia mtu
kuwa na presha ya kawaida.
Napenda nichukue nafasi hii kuwafahamisha kuwa, bila kubadili mfumo wa maisha
ulionao, hata ukikusanyiwa dawa nzuri za dunia nzima kwa kutibu maradhi yako
hutopata uzima wowote. Kubadili mfumo wa maisha si katika kuishughulikia presha
tu, bali kwa maradhi yote ndio
Tiba sahihi. Nini dawa zinafanya ?. Dawa zinalazimisha kuurudisha
mfumo katika hali yake ya kawaida tu. Baada ya dawa kutoa msaada wake huu,
kinachotakiwa kwako wewe kuendeleza mfumo huo unaofaa ambao dawa zimekurudishia
tena.
Kwa kutegemea sababu za kupata presha uliyonayo, unaweza kuchukua hatua
zifuatazo :
§ Kunywa maji mengi, kuacha kunywa pombe, Kula
vyakula kiafya (kula nafaka, matunda, mbogamboga, kula mifupa ya samaki na hata
ya ndege[kuku,njiwa nk]) Tupendelee kuku wa kienyeji zaidi. Ikiwa kuongeza
chumvi katika chakula, basi usizidishe vijiko viwili vya chai kwa siku na ni
vizuri sana upate ushauri kwa daktari.
§ Kujenga utamaduni wa kuinuka taratibu ulipo kaa
ua kulala. kulalia mto, ikiwa unapenda kunalalia ubavu, pendelea
kulalia upande wa kulia (kila unapozungumzia presha, basi jambo la kwanza la
kukumbuka ni moyo, moyo wako uko upande wa kushoto, kitendo cha kulalia upande
wa kushoto kinaweza kuupa tabu moyo katika utendaji wake wa kazi).
§ Kuwa na tabia ya kula chakula kidogo katika mlo
wako. Kufanya hivyo kunasaidia presha yako kutoshuka baada ya kumaliza
kula. Jipangie utaratibu wa kula mara kwa mara ili uweze kula chakula cha
kutosha. Punguza kula vyakula vyenye uwanga kwa wingi kama vile, mbatata, wali
na mikate. Kula chakula pamoja na chai au kahawa. Ni vizuri haya yote
utakayoyafanya ukawasiliana na daktari kabla.
Kinga ya presha ya kushuka.
Ikiwa wewe ni mzima au tayari una presha ya kushuka, daktari atakushauri hatua
za kuzuia isitokee au isiendelee au kuipunguza. Hatua hizo ni pamoja na :
1. Kuacha unywaji wa pombe.
2. Kuepuka kusimama muda mrefu ( hasa ikiwa tayari una NMH)
3. Kunywa maji kwa wingi
4. Kuinuka taratibu kutoka ulipokaa ua kulala
5. Kuvaa mavazi ya kubana miguuni (ikiwa tayari unayo)
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
-
No comments:
Post a Comment