
Watu
wengi wamekuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya uhusiano kati ya
mafuta ya taa (kerosene) na hali au hisia za kimapenzi (libido). Wapo
wanaosema kuwa mafuta ya taa hupunguza hisia za kimapenzi, pia wengine
wanaona hakuna uhusiano wowote wa vitu hivi viwili. Yawezekana
hujawahi kukutana na kisa hiki, ila kwa walio wengi waliowahi kusoma
shule za bweni (boarding schools) nadhani kitu hiki siyo kigeni kwaoJe ukweli ni upi?
Ukweli
ni kwamba hakuna uthibitisho wowote kisayansi unaoonesha kwamba Mafuta
ya taa yanapunguza hisia au hamu ya kufanya mapenzi(libido),hakuna
ushahidi wowote wa kitaalamu unaoonesha kama mafuta ya taa yakiingia
mwilini huleta mabadiliko yoyote katika hormones.
Mafuta
ya taa hutumika kusaidia kuongeza utendaji kazi wa utumbo(bowel
movements) hivo kusaidia watu wenye tatizo la kutopata choo kupata.
Lakini
pia kitaalamu kula kiwango kikubwa cha mafuta ya taa pia ni sumu
mwilini inaweza kupelekea utumbo kutofanya kazi vizuri( kuziba kwa
utumbo)
No comments:
Post a Comment