Njia ya kutumia kalenda ya uzazi wa mpango ni mojawapo ya
njia ambazo hukadiria ni wakati gani mwanamama huweza kupata ujauzito, na
misingi yake ni uelewa na kuweka rekodi ya mizunguko ya hedhi ya miezi
iliyopita.
Muhimu ya
kuzingatia
Mwanamama anaweza kutumia Njia ya wanaopata siku za
hedhi za kawaida kama siku zake za mzunguko wa hedhi ni kati ya siku 26 hadi 32
kwa urefu. Kama mwanamama atakuwa na mizunguko ya hedhi zaidi ya 2 ndani ya mwaka
ambayo ni mirefu au mifupi ukilinganisha na mizunguko ya kawaida ya hedhi, njia
hii ya kawaida ya kalenda haitaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Vifaa vinavyohitajika
Kalenda, kalamu, simu ya mkononi (ukipenda)
Jedwali la maelekezo
Fuatilia na weka
rekodi ya siku za mizunguko ya hedhi.
|
|
Epuka tendo la ndoa
bila kinga kati ya siku ya 10 hadi siku ya 20.
|
|
Tumia viweka
kumbukumbu
|
|
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG



No comments:
Post a Comment