Mke wa Rais Donald Trump, Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo katika hospitali ya Walter Reed Medical Center.
Kwa mujibu wa msemaji wa Melania, Stephanie Grisham amesema upasuji huo umekuwa wenye mafaninikio makubwa na hakukuwa na matatizo yoyote yaliyojitokeza.
Naye Rais Trump amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter huku akiwashukuru wote waliokuwa wakimuombea mkewe.
Taarifa za kufanyiwa upauaji huo zilitolewa na Ikulu ya Marekani Jumatatu hii huku ikidaiwa kuwa ataendelea kubakia hospitali kwa wiki yote hii ili kuweza kupata nafuu zaidi.
No comments:
Post a Comment