HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » MZEE WA MIAKA 104 AOMBA MSAADA WA KUJIUA


 Huyu ni mwanasayansi kutoka Australia, David Goodall aliyezaliwa katika Jiji la london April 4, 1914 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 104.(karne 1)

Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel nchini Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.

Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.

Kwahivyo siku ya leo Alhamisi ya tarehe 10, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.

Kitanda ni kitanda ambacho mwanasayansi huyu Mkongwe anatarajiwa kukilalia wakati anakatisha uhai wake.

Dawa iitwayo sodium pentobarbital ambayo itajazwa kwenye sindano na kumruhusu mwanasayansi huyo kujidunga ili kukatisha uhai wake.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: