
KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo
zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye
tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo
cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda.
Mwanaume endapo atakuwa na
korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo
kubwa.
Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za
kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili
lakini
akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali
tuliyoelezea katika
toleo
lililopita.
Mwanaume mwenye korodani moja
anaweza
kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa,kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona
uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana
korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo
wa
kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja
kuliona katika makala zijazo.
Maumivu ya korodani hutokea katika
korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au
maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda
mfupi,yanakuwa
makali
kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena
yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo
siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha. Maumivu ya korodani
yanaweza kuwa makali kiasi
kwamba
yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa,
ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s
gangrene’ au inatamkwa ‘Fonias gangrini’.
Vilevile
inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu
makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa ‘Testicular
Torsion’. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu
ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua
takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla
huwa
hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi
fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi ‘Vesectomy’ lakini baadaye
hupoa. Vilevile
husababishwa
na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits,
Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi
vya mwanaume na husababisha ugumba.
Tutakuja
kuona katika matoleo yajayo. Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa
ndani,pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza
kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, mbegu za
kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia
tutakuja kuyaona.
Yote
haya humsababishia mwanaume ugumba. Maumivu pia husababishwa na kuumia korodani
au baada ya kufanyiwa upasuaji kama tulivyokwishaona hapo awali. Maumivu
yatokanayo na korodani au kende kujinyonga huwa makali sana na korodani
zikiguswa
huuma
sana na kawaida huendelea hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.
Maumivu ya korodani (Testicular pains)-2
Naelezea maumivu yatokanayo na korodani au kende kujinyonga
ambapo nilisema huwa
makali na kurodani zikiguswa huuma sana
na kawaida huendelea hivyo kwa saa zisizozidi sita. Leo naendelea ili
uweze kujua matatizo hayo kwa undani.
Kwa kawaida maumivu ya korodani hupanda
juu zaidi na kuacha mfuko wake mtupu. Tatizo hili huwatokea zaidi vijana
chini ya umri wa miaka 25 ingawa pia inaweza kutokea katika umri zaidi ya
huo.
Tatizo hili huhitaji upasuaji wa dharura.
Wakati mwingine tatizo hili hutokea kwa
korodani kuwa na tabia ya kupanda au kushuka, ikishuka
mgonjwa
hupata nafuu, hali huendelea vivyohivyo kwa vipindi fulani. Hali hii inapotokea
mgonjwa hutapika na kukosa nguvu.
Maambuziki
ya korodani pia mtakuja kuyaona kwa undani baadaye lakini pia huambatana na
maambukizi katika mkojo au ‘UTI’ na homa. Huwa makali kwa vipindi. Kisonono na
gono huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.Uvimbe kama jipu wa korodani au
Fonias gangrini kama tulivyoona hapo awali ni mbaya kwani korodani inakuwa kama
inaoza halafu tatizo hilo lina tabia ya kusambaa kuelekea uvunguni jirani na
njia
ya haja kubwa. Uvimbe huwa kama busha au jipu kubwa lakini ndani yake hakuna
maji wala usaha.
Tatizo
hili pia tutakuja kuliona kwa undani kwani nalo huathiri wanaume wengi na ni
tatizo kubwa ambalo mwanaume yeyote ni rahisi kupata pia hupoteza uwezo wa
kuzaa.
KORODANI
KUSHINDWA KUFANYA KAZI (TEST CULAR FAILURE)
Kazi
ya korodani ni kuzalisha vichocheo au homoni za kiume na mbegu za kiume.
Mwanaume anatakiwa awe na korodan mbili ingawa ukiwa na moja pia inaweza
kufanya kazi kama ni nzima, inatakiwa
kama unayo moja nenda hospitali ukapimwe kuthibitisha ubora wake na uwezo wake.
Katika hali isiyo ya kawaida wapo
wanaume wenye korodani tatu.
Ukishakuwa na hali hii ni vema ukapimwe
hospitali.
Matatizo
mengi ya korodani tumeshayaona kwa kina katika matoleo yaliyopita
na tunamalizia kuyaona leo huku tukiangalia na mada hii.
Matatizo ya korodani kama tulivyoyaona
ndiyo matokeo ya kushindwa kufaya kazi.
Korodani kushindwa kufanya kazi tunaweza
kuweka katika makundi mawili, kwanza ni hali ya
uwezo
wake kuwa mdogo tangu balehe ‘Hypogonadism’ na tatizo linaweza kutokea ukubwani
yaani baada ya balehe au utu uzima ‘secondary hyponadism.’
Tatizo linapotokea katika utu uzima
huambatana na upungufu wa nguvu za kiume, kusinyaa korodani na uume kuwa mfupi
au mdogo. Hii ni kutokana na korodani kushindwa kuzalisha
vichocheo au homoni za kiume kama tatizo
ni tangu balehe, basi hali ya matatizo makubwa hutokea katika mfumo wa uzazi na
mwili kwa ujumla. Hayo ni baadhi tu ya matatizo ila mengi tutaendelea kuyaona.
CHANZO CHA TATIZO
Korodani
kushindwa kufanya kazi husababishwa na matatizo mengi kama vile matumizi ya
madawa baadhi yake ya hospitali kwa muda mrefu hasa kwa wanaume mfano dawa za
jamii ya Glucocorticoids, Ketoconazole, na madawa ya kulevya hasa bangi.
Matatizo
ya kuzaliwa nayo Chromosome Problems magonjwa yanayoathiri korodani mfano Mumps
na joto kali na la muda mrefu katika korodan. Kuumia moja kwa moja kwa korodani
Direct Injury na kuvimba na kujinyonga kwa korodani Testicular Torsion.
Watu
ambao wapo katika hatari kubwa korodani zao kuja kushindwa kufanya kazi ni wale
ambao hufanya shughuli zinazoumiza korodani zao taratibu na kwa muda
mrefu mfano waendesha pikipiki
au
bodaboda katika barabara mbovu kwa muda mrefu, huwa kitaalamu huziumiza
korodani zao Constant low level injury to the Scrotum na wale ambao wana
korodani moja au hawana kabisa.
DALILI ZA TATIZO
Endapo
korodani zako zinashindwa kuzalisha mbegu za kiume utajikuta unaishi na mke kwa
zaidi ya mwaka mmoja na mnafanya tendo la ndoa kwa lengo la kutafuta mtoto na
mnakosa.
Endapo korodani zinashindwa kuzalisha
homoni za kiume basi utakuwa na dalili zifuatazo, kama ni mtoto anakuwa
harefuki anaendelea kuwa mfupi huku umri unaenda, matiti ya mtoto wa kiume au
kijana yanakuwa makubwa Gynecomastia
mwili hauwi na misuli imara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, unakuta vinyweleo
vya kwapani na sehemu za siri havioti au kama vilishaanza kuota havikui
hata
kwa zaidi ya mwaka, huoti ndevu na kubadilika kama mwanaume, uume haukui na
korodani zinasinyaa na kuwa kama za mtoto. Sauti haiwi nzito.
UCHUNGUZI
Matatizo
ya viungo vya uzazi huchunguzwa katika hospitali za wilaya na mkoa, uchunguzi
wa awali hufanyika kwenye vituo vya afya.
Vipimo mbalimbali hufanyika kadiri
daktari atakavyoona inafaa.
USHAURI
Matibabu
huchukua muda mrefu baada ya uchunguzi wa kina. Matibabu ya dharura hufanyika
pale kunapokuwa na maumivu makali.
Ni vema kuepuka maambukizi hasa ya
magonjwa ya zinaa na kuwahi hospitali pale unapohisi una tatizo.
No comments:
Post a Comment