Mbunge wa Momba (Chadema), David Salinde amesema Wizara ya Fedha na Mipango ndio adui namba moja wa maendeleo ya Taifa na kushauri Bunge liichukulie hatua ili kutekeleza maagizo yake.
Silinde akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19, jana Juni 4, 2018 bungeni, alisema: “Kwa lugha nyepesi kabisa, adui namba moja ni Wizara ya Fedha na Mipango. Wizara ya fedha inashindwa kutoa fedha ambazo zipo kisheria.”
Silinde amesema ukiangalia ripoti za CAG, wizara imekusanya fedha lakini haipeleki sehemu husika.
“Leo watu wa korosho wanalalamika wamekusanya Sh91 bilioni, wamepelekewa Sh10 bilioni,”alisema na kuongeza; “Wana sababu moja tu, uhakiki na ndio kichaka cha kujifichia kupeleka fedha. Mawaziri wanakuja hapa wanalia. Wao wajibu wao kukusanya na kupeleka. Hivi hawa wanaitakia mema nchi hii”
No comments:
Post a Comment