Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na uongozi wa juu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) alipotembelea mamlaka hiyo na kupata taarifa ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya kisasa ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Daniel Malanga akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile kuhusu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya kisasa ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo gharama za mradi ni takribani shilingi Bilioni 78.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akipata amaelezo kutoka kwa Meneja Mradi Stephen Mwakasasa kuhusu ujenzi wa majengo ya kisasa ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akitolea ufafanuzi kuhusu namna Chuo hicho wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile alipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile (Mb) ametembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kukutana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na uongozi wa juu wa Mamlaka.
Katika ziara hiyo, Mhe. Kihenzile amepokea ambapo Serikali imeamua kugharamia mradi wote na unategemewa kukamilika kwa kipindi cha miaka mitatu.
Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Daniel Malanga amesema sasa hatua iliyofikiwa ni mchakato wa kumpata mkandarasi mjenzi na Mara baada ya hatua hii kukamilika ujenzi utaanza mara moja.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Mhe. Kihenzile amesisitiza hatua zote zizingatie muda ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati.
"Sina shaka na weledi wa TCAA katika utekelezaji wa majukumu mliyokasimiwa, wito wangu ni kuwa mzingatie maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ana malengo makubwa ya kuhakikisha sekta ya Anga inakua nchini" alisema Mhe. Kihenzile
Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwniyimvua aliishukuru serikali kwa kuubeba kwa uzito mradi wa uboreshwaji wa CATC kwa kutenga fedha ili kuhakikisha unatekelezwa kikamilifu.
Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania ni moja kati ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Mkutano ukiendelea
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiookea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwniyimvua alipomaliza kuongea na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na uongozi wa juu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) alipotembelea mamlaka hiyo na kupata taarifa ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya kisasa ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) .
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na viongozi mbalimbali wa mamlaka hiyo wakati wa ziara yake.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiendelea na ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC)
No comments:
Post a Comment