Lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa upangaji wa bajeti, mipango na sera zinazozingatia jinsia, miongoni mwa watoa maamuzi pamoja na kutambua mapengo yaliyopo kwenye eneo la ushawishi na kujenga uwezo wa stadi za utetezi kwa siku za usoni.
Pia ni muhimu kuimarisha ujuzi wa watoa maamuzi wa ndani katika kutekeleza sera na programu zinazozingatia jinsia, ikiwa ni pamoja na kufanya uchambuzi wa kijinsia, kuweka shabaha zinazozingatia jinsia, na ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo pamoja na kutambua somo lililopatikana, changamoto na mafanikio ya shughuli zilizotekelezwa.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia katika muktadha wa uandaaji wa Bajeti kwa mrengo wa kijisia na masuala muhimu ya kijinsia ya kuzingatia wakati wa uandaajiwa Bajeti wakati wa mafunzo ya Watendaji na Maafisa maendeleo ya jamii yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watendaji na maafisa maendeleo ya jamii wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wataalamu kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakati wa mafunzo ya Watendaji na maafisa maendeleo ya jamii yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Majadiliano yakiendelea yanayohusu dhana na Bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia na uongozi wenye mrengo wa Kijinsia wakati wa mafunzo ya Watendaji na maafisa maendeleo ya jamii yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment