Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) mwaka 2024 kwa kupandisha bendera ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Banana-Ukonga jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na watumishi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi amesema desturi ya sekta hii ya usafiri wa anga kila ifikapo Desemba 07 kila mwaka huwa wanaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga. Na kuongeza kuwa kwa mwaka 2024 Mamlaka imetekeleza mambo mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho ya ICAD.
"Kuanzia Desemba 01 mpaka 06 TCAA kwa kutumia watumishi wake walitoa elimu katika Shule ya Sekondari ya Kibasila, Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, Shule ya Sekondari ya Makongo na Shule ya Sekondari ya Kwembe.
Aliongeza katika wiki hiyo pia watalaam wa TCAA akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA walifanya ziara kwenye vyombo vya habari vya radio na televisheni na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala kadhaa ya Usafiri wa Anga, fursa zinazopatikana pamoja na kukinadi Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania( CATC).
Bw. Msangi alifafanua kuwa lengo hasa la siku hii ni kukumbushana majukumu yetu na kuhakikisha tunasimamia shughuli za usafiri wa anga na kuhakikisha kwamba anga letu na hata anga la nchi za jirani linaendelea kuwa salama
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akipandisha Bendera ya hirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Banana-Ukongo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Banana-Ukongo jijini Dar es Salaam.
Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally akizungumza kuhusu namna mamlaka hiyo ilivyoweza kushinda tuzo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Banana-Ukongo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa TCAA wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani yaani International Civil Aviation Day (ICAD) yaliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka hiyo Ukonga- Banana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment