HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

DIWANI DEBORA SANGA AZINDUA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ WILAYA YA ILALA ILIYO CHINI YA KITUO CHA MSAADA WA SHERIA WLAC

    Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kulia) akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa na Mwanasheria  WLAC, Wigayi Kisandu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. Picha na Muhidin Sufiani  Mafoto Blog
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akimkabidhi  zawadi ya vitabu Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan,  wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika  Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akiwakabidhi  zawadi ya vitabu Wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Zawadi,  wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika  Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
 Mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika  Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 
Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,wakiigiza mbele ya mgeni rasmi na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan, akizungumza wakati akitoa ushuhuda wa Vitendo vya Unyanyasaji kwa Wanawake alivyowahi kuvipitia. Consoler alikuwa kitoa ushuhuda huo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa meza kuu.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Sekondari  waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,washambulia jukwaa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

MKUU WA MKOA AMGOMEA WAZIRI MAGHEMBE

Uamuzi uliofanywa wiki iliyopita na Waziri wa Maliasili na Utalii, Professa Jumanne Maghembe wa kuagiza kuendelea mchakato wa kulitenga eneo la pori tengefu la Loliondo umepingwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Badala yake, RC Gambo ameagiza Kamati ya wataalamu iliyoundwa kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Khasimu Majaliwa inayochunguza chanzo cha mgogoro wa Loliondo iendelee na kazi iliyopewa na hatimaye itoe mapendekezo yake ya namna ya kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miongo miwili.

Gumbo alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa wadau wa vyombo vya habari   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Alisema hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kukosoa au kusimamisha maagizo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais. 

RC Gumbo alionekana dhahiri kuwa amekerwa na kukasirishwa na uamuzi wa Waziri Maghembe wa kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Loliondo na   kutoa maagizo ya kugawa eneo la kilometa za mraba 1500  kuokoa Hifadhi ya Serengeti.

Alisema uamuzi uliotolewa na waziri  huyo ni ushauri kwa kamati yake na jambo linalozusha sintofahamu juu ya mwenye mamlaka zaidi kati ya Waziri na Mkuu wa Mkoa . 

“Hakuna kiongozi mwingine yeyote mwenye kukosoa maagizo au maelekezo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais.

“Sisi kauli ya waziri tunaichukulia kama ushauri ambao unaweza kutolewa na mwananchi yeyote, ” alisema.

Alisema ni lazima kamati ya wataalamu aliyoundwa ikamilishe kazi yake ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kuhusu mipaka, vyanzo vya maji, maeneo ya ufugaji, uhifadhi, mipaka ya vijiji na hatimaye  kuwasilisha mapendekezo yake serikalini   yafanyiwe kazi na si vinginevyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa na uelewa na umakini wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kulitambua na kufuatilia eneo la pori tengefu.

RC Gumbo alisema inaelekea  wataalamu wa wizara hawana uelewa wowote kuhusu kinachoendelea Loliondo.

“Wizara inazungumzia pori tengefu lakini tayari kuna mji pale, hata eneo la kilometa za mraba 1500 wanazosema tumewauliza inaanzia wapi na kuishia wapi hawajui.

"Hata aliyechora ramani naye hajui mipaka ndiyo maana nasema tuache kamati imalize kazi yake," alisema.

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KAGERA (RAS) KAMISHNA DIWANI ATHUMANI LEO IKULU DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Kamishna Diwani Athumani mara baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa,  Bw. Waziri Kipacha akimuongoza  Kamishna Diwani Athumani kula  kiapo cha uadilifu cha viongozi wa umma   baada ya kuapishwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Kamishna Diwani Athumani pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama umma   baada ya Kamishna Diwani kuapishwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA WA DCI- DIWANI ATHUMAN KUWA RAS WA KAGERA PIA AMETEUA WENYEVITI WA BODI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI AKIWEMO JAJI WARIOBA.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Diwani Athuman

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA UPELELEZI MAKOSA YA JINAI (DCI) DIWANI ATHUMANI LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw. Diwani Athumani

DIWANI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHOMWA MKUKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Diwani wa Kata ya Kaloleni eilayani Kiteto mkoani Manyara, Christopher Parmet amenusurika kufa baada ya kuchomwa mkuki na wafugaji wa eneo hilo wakati akifukuza mifugo iliyovamia shamba lake.
Diwani huyo ambaye ni katibu mwenezi wa CCM wilayani Kiteto na katibu wa mbunge wa jimbo hilo, Emmanuel Papian na hivi sasa amelazwa kwenye hospitali ya wilaya hiyo akipatiwa matibabu.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Papian alisema afya ya Parmet inaendelea vizuri baada ya kuongezewa damu kwani alivuja damu nyingi baada ya kuchomwa mkuki kiganjani.
Papian alisema diwani huyo alijeruhiwa jana jioni alipofika shambani kwake kwa ajili ya kuwalipa vibarua wake watatu ambao pia walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.
Baada ya tukio hilo diwani huyo alipiga simu kwa mkuu wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo kwa ajili ya kutoa taarifa ndipo mkuu wa polisi wa wilaya akatuma gari lililowachukua na kuwafikisha hospitalini.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alisema yupo nje ya nchi hivyo asingeweza kuzungumza tukio hilo.
Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dk Lupembe alithibitisha majeruhi hao kulazwa kwenye hospitali ya wilaya hiyo na kuwa wanaendelea kupata matibabu.

CHADEMA YALAANI DIWANI KUSWEKWA RUMANDE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Katibu wa CHADEMA jimbo la Arumeru Mashariki Elisa Stephen Mungure (Kulia) akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda (kushoto) nje ya Mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu jana mara baada ya kuwekwa rumande kwa saa 48 na mkuu wa wilaya ya Arumeru ambapo jana alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana

      Na Woinde Shizza, Arusha 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Arumeru Mashariki kimelaani vikali kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti kumuweka rumande Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda kwa saa 48 na kudai kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya madaraka. 

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru Elisa Stephen Mungure amesema kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji dhidi ya viongozi wa upinzani ambao wamekua wakikamatwa mara kwa mara na kuwekwa rumande . 

Mungure alisema kuwa mbinu hiyo imekua ikitumika kwa hila ili kudhoofisha na kuua upinzani hivyo chama chake kimejipanga kukabiliana na hila hizo za kisiasa. 

“Diwani wa Kata ya Embaseny alitakiwa kuripoti katika kituo cha polisi cha Usariver septemba 20 mwaka huu ndipo alipokutana na Amri ya Mkuu wa Wilaya ya kuwekwa ndani kwa masaa 48 bila kuhojiwa ,jana alifikishwa mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu na kutuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mradi wa Kuku Kukua ambao Diwani huyo siyo muhusika ,tunamshukuru Mungu amepata Dhamana” Alisema Mungure 

Akizungumza baada ya kupata Dhamana katika mahakama hiyo Diwani huyo Gadiel Mwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki alisema kuwa Mkuu wa Wilaya alifanya ziara katika kata yake na kuzungumza na Wananchi ,baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM walimshutumu kuwa anahusika na mradi huo alipotaka kujitetea alinyimwa nafasi hiyo na kuamriwa kufika kituo cha polisi asubuhi na mapema ndipo alipokutwa na masaibu hayo. 

Mwanda alisema kuwa misigano ya kisiasa inayotekea inalenga kuzorotesha juhudi za maendeleo ambazo amekua akizifanya kwa kushirikiana na wananchi jambo ambalo litawaathiri wananchi wengi hivyo amewataka wananchi kuendelea na juhudi hizo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya kisasa. 

Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo Ester Swai na Agnes Elia wamesema kuwa kukamatwa kwa viongozi kila mara kunazua hali ya taharuki miongoni mwa wananchi hivyo wamezitaka mamlaka husika kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

DIWANI WA CHADEMA TEMEKE AFUKUZWA UANACHAMA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama Diwani na Mwenyekiti wake kutoka kata ya Kurasini, Matiti Claudian Togocho kutokana na kashfa ya ufisadi wa zaidi ya shilingi milioni 400 alizozipata kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa iliyotolewa na Benard Mwakyembe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke imeeleza kuwa mnamo November 23 2015, Diwani huyo akiwa na wenzake wanadaiwa walitengeneza hati feki ya nyumba tano za James Makundi aliyekuwa mpangaji kwenye nyumba zake kisha kufanya hujuma ya kuvunja nyumba hizo kwa amri ya uongo ilitolewa na wakili kishoka wa Samora Avenue badala ya amri ya mahakama ikiwa ni kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa mwekezaji ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.

Diwani huyu pia anahusishwa na matukio mengine mawili ya udhulumaji wa zaidi ya shilingi milioni 140 za mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni wakati kesi ikiwa mahakamani pamoja na fedha za fidia za Paulina Shaban na wajukuu zake ambao Diwani huyo alisimamia nyumba zao kubomolewa.

"Kutokana na maamuzi ya chama baada ya kujiridhisha na makosa yake na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, mamlaka za mwisho zimefikia maamuzi ya kumvua uanachama wake hivyo atakuwa amepoteza sifa za kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mivinjeni pamoja na nafasi yake ya Udiwani kata ya Kurasini." Alisema Benard Mwakyembe