Gari la TANESCO Iringa likitoa msaada wa lori lililopinduka usiku wa leo eneo la Mwangata Iringa
Watu
kadhaa wamenusurika kifo usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mwangata
katika Manispaa ya Iringa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuacha
njia na kupinduka .
Ajali
hiyo mbaya imetokea eneo la kona ya Mwangata ambapo inadaiwa kuwa
dereva wa lori hilo ambalo lilikuwa limebeba kokoto kuendesha lori hilo
bila kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutaka kukata kona huku
akiwa na spidi zaidi ya 100 hali iliyopelekea lori hilo kuacha njia na
kupinduka.
Mbali
ya abiria waliokuwemo katika lori hilo kunusurika kifo pia wakazi wa
nyumba moja iliyopo jirani na barabara eneo hilo pia wamenusurika
kutokana na lori hilo kutaka kugonga ukuta wa nyumba hiyo na iwapo
lisingepinduka basi lingeweza kuvunja ukuta na kuingia moja kwa moja
katika nyumba hiyo .Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha na
dereva wa lori hilo anadaiwa kukimbia baada ya ajali .
No comments:
Post a Comment