“Hadi sasa tunamshikilia mama yake na watu wengine
wote wakazi wa Kijiji cha Mwanyonye. Ngariba alifanikiwa kutoroka lakini
tumeanzisha msako mkali kumkamata ili tuwafikishe kwenye mahakamani,”
alisema.
WATU wawili mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwamo la mtoto mwenye umri wa miezi minne kupoteza maisha baada ya kukeketwa.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida, Linus Sizumwa alimtaja mtoto aliyefariki dunia baada ya
kukeketwa kuwa, ni Shamila Saidi.
Alisema tukio hilo la kinyama lilitokea Oktoba 27,
mwaka huu saa 10:00 alfajiri Kijiji cha Mwanyonyi, Tarafa ya Ilongero,
mkoani Singida.
Alisema siku ya tukio, mama mzazi wa mtoto huyo
alimpeleka mtoto wake kukeketwa kwa ngaraiba, ili aweze kupona ugonjwa
wa kuharisha na kutapika. Magonjwa hayo yanadhaniwa kusababishwa na
ugonjwa wa lawalawa.
Sizumwa alisema baada ya kukeketwa, mtoto huyo alivuja damu nyingi na kusababisha kifo chake.
“Hadi sasa tunamshikilia mama yake na watu wengine
wote wakazi wa Kijiji cha Mwanyonye. Ngariba alifanikiwa kutoroka
lakini tumeanzisha msako mkali kumkamata ili tuwafikishe kwenye
mahakamani,” alisema.
Katika hatua nyingine, Sizumwa alisema Samwel
Majilala mkazi wa Kijiji cha Kideka, Kata ya Puma, Wilaya ya Ikungi
ameuawa na vijana wenye hasira kwa kinachodaiwa ni kumpiga baba yake
mdogo.
Alisema mauaji hayo yamechangiwa na ugomvi wa
kugombea Sh600,000 ambazo babu yake alilipwa fidia ya kupisha ujenzi wa
umeme wa upepo.
“Katika fidia hiyo, mtoto alipata mgawo wa
Sh200,000. Mjukuu wa mzee naye alianza kuomba kupewa mgawo. Samwel baada
ya kushindwa kupata mgawo huo alianza kumpiga baba yake kwa madai kuwa
ni kikwazo cha yeye kukosa,” alisema.
Alisema Samwel baada ya kumpiga baba yake mdogo,
alitoroka na kukimbilia Kijiji cha Dung’unyi ambako alifuatwa na kundi
la vijana na alipokamatwa, alipigwa hadi kusababisha kifo chake.
Kamanda Sizumwa alisema hadi sasa wanawashikilia watu saba kuhusiana na mauaji hayo na msako zaidi unaendelea.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment