HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » R.I.P MHADHILI WETU DEOGRATIUS KAMILIUS

Viongozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kuanzia Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrisa Kikula, Naibu Makamu Mkuu wa Elimu,Utafiti na Ushauri Prof Ludovick Kinabo na Naibu Makamu Mkuu Mipango,Fedha na Utawala Prof Shabani Mlacha,Dean wa collage ya Social Science, Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma, Pamoja na Wanafunzi wa Kozi Mbalimbali leo wamehudhuri Kuaga Mwili wa Marehemu wa Aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Deogratius Camillius ambaye amefariki alfajili ya tarehe 24/10/2012 kwa Mshtuko wakati akiangalia Mpira na Jamaa zake. 
 
 
 Baadhi ya Ndugu, Jamaa wa Marehemu wakiaanda kwaajili ya Kuaga Mwili wa  Marehemu
 
Ibada ya Kuombea Mwili wa Marehemu Deogratius Camillius ikiendelea huku waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza alilolazwa marehemu wakati wa ibada nyumbani kwake kisasa mjini Dodoma leo. Kabla mwili wake haujasafirishwa kupelekwa Mkoani Morogoro Kwaajili ya Mazishi.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika majonzi na mshangao wa hali ya juu kwani iliwachukua muda mrefu sana kuamini kilichotokea
Kiongozi wa Dini akiendelea kuongoza Ibada ya Kumuombea Marehemu kabla mwili wake haujasafirishwa kuelekea Morogoro kwaajili ya Mazishi
Jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu Kabla mwili wake haujasafirishwa kupelekwa Mkoani Morogoro Kwaajili ya Mazishi.
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika majonzi
  Mmoja wa viongozi wa UDOMASA MR MKANACHI akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya UDOMASA
 Principal wa College ya Social Science and Humanities Prof. Casmir Rubagumya akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Uongozi na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma leo katika msiba uliofanyika Nyumbani Kwa Marehemu Mjini Dodoma kabla ya Mwili wake haujasafirishwa kupelekwa Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi.
 
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma, Ndugu, Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwenye Msiba wa Marehemu Deogratius Kamillius ambaye amefariki leo majira ya asubuhi wakati akiwa hospitalini
 
 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu DEOGRATUS  KAMILIUS  likipandishwa kwenye gari tayari kwa kusafirishwa kuelekea mkoani morogoro kwa ajili ya mazishi
  Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Deogratius Kamilius Likiwa tayari kwaajili ya Safari ya Kuelekea Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi.
 
Picha Na Sulemani Magoma wa Lukaza Blog

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 
CHANZO: LUKAZA BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: