MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau, kutokuwa katibu wa kamati ya ukaguzi wa hesabu za ndani wa shirika hilo.
Zitto alitoa
agizo hilo jana jijini Dar es Salam wakati watendaji wa shirika hilo
walipokuwa katika mahojiano na kamati hiyo na kushauri kutafutwa mtu
mwingine awe katibu wa kamati hiyo.
“Nafikiri
yalikuwa yanafanyika makosa makubwa, mkurugenzi mkuu kuchukua nafasi ya
katibu wa kamati ya hesabu za ndani na kujikagua mwenyewe … sasa
ninaagiza kwamba aondoke ichukuliwe na mfanyakazi mwingine,” alisema
Zitto.
Zitto
alisema hakuna sheria na si haki kwa kiongozi yeyote kutumia nafasi yake
au kuchaguliwa kujichunguza, bali kazi hiyo inapaswa kufanywa na
wafanyakazi wengine.
Katika hatua
nyingine, Zitto aliitaka NSSF kuielimisha jamii na kuboresha huduma ya
mafao ya bima ya afya ambayo yalianza miaka michache iliyopita.
Aliwataka kuwatumia wasanii kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya namna ya kujiunga na kueleza namna mafao ya afya yanavyotolewa.
Pia, Zitto
aliitaka NSSF kuangalia namna ya kutengeneza kadi za wanachama tegemezi
(watoto), ili kuondoa usumbufu unaojitokeza pale wanapotaka kupatiwa
matibabu.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment