MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha Lamadi, wilayani
Busega mkoani Simiyu, juzi walifurika katika Kitongoji cha Mabulugu
kumshuhudia mwanamke Ngulima Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku
mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani
humo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Habari zaidi kutoka katika kitongoji hicho
zinasema mwanamke huyo bado amefungiwa ndani ya nyumba yake akifanyiwa
dawa za kienyeji ili arudie katika hali yake ya kawaida, kwani kwa sasa
anaonekana kama zezeta.
“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba
za usiku wa kuamkia leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili
atoke, akapiga sana mlango...wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia
hadi sasa bado yumo ndani na usiku alipewa chakula akala na asubuhi
amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa mwanamke huyo.
Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa kienyeji
amekwisha kuja kwa ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze kurudia
hali yake na kwamba amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka maiti kwenye
nyumba ya mtuhumiwa huyo, kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi
alithibitisha tukio hilo, lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za
kishirikina.
Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika
eneo la tukio kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni
jana, maiti ya mwanamke huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.
Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.
Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe Ngitu
Masisanga na mama yake mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua
ghafla juzi baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula
nyumbani kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
Alisema cha ajabu ni kwamba wakati wamelala
nyumbani kwa marehemu sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku
marehemu alitokea akiwa uchi.
Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na
kutazama picha hizo na kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo
alichukua tochi iliyokuwa ikiwaka na kuizima.
Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya kukimbia
nje tulimzuia yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio
tukakimbilia nje, licha ya kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu
ufunguke ila na yeye aweze kutoka nje, kuna mtu amefanya dawa za
kienyeji ndio tunasubiri majibu.”
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkula, Cymthia Mugussi alielezea jinsi mgonjwa huyo alipopokelewa hospitalini hapo na kwamba baada ya kumchunguza walibaini kuwa na upungufu wa damu, lakini baada ya kuchukua vipimo na kabla ya majibu kutoka alifariki dunia.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkula, Cymthia Mugussi alielezea jinsi mgonjwa huyo alipopokelewa hospitalini hapo na kwamba baada ya kumchunguza walibaini kuwa na upungufu wa damu, lakini baada ya kuchukua vipimo na kabla ya majibu kutoka alifariki dunia.
Hata hivyo wananchi wakiwamo wana nzengo wa eneo
hilo waliendea maiti na kuileta kijijini hapo, ambapo ilikuwa tayari
imebadilika sana kwa kuvimba tumbo kama mtu mwenye mimba na usoni
kuonekana kama mzee tofauti na awali marehemu alipokufa na kuhifadhiwa
hospitalini hapo.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwamo
mwenyekiti wa kitongoji hicho Amos Mapema, na mwenyekiti wa wana zengo,
wanaeleza tukio hilo kwamba ni la tatu kutokea kwa muda mfupi katika
kitongoji hicho, ambapo watu wamekuwa wakifariki ghafla.
Aidha, kutokana na hali hiyo wananchi waliazimia
kuwa sasa wanawake ndio wawe wanachimba kaburi wakiwatuhumu kuwa wao
ndio wachawi.
Diwani waka ya Lamadi alisema kuwa hadi jana saa
6:00 mchana maiti ya mwanamke huyo ilikuwa haijazikwa na kwamba polisi
walienda katika eneo la tukio, ili kuwaambia wananchi waizike katika
eneo la serikali.
Aidha habari za kuaminika zinasema kuwa baadaye
wanazengo walibeba maiti ya mwanamke huyo na kuipeleka katika nyumba ya
mtuhumiwa huyo ambamo sasa inadaiwa kuwa imevimba sana na imeachama na
mdomo uko wazi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI



No comments:
Post a Comment