CARIBBEAN, Colombia
KUZAA watoto ni hatua inayofurahiwa na wanandoa wengi na kwa kawaida, kina mama wengi huwa na furaha wanapojifungua watoto wenye afya njema na walio kamili.
Lakini, hali haipo hivyo kwa Ann Feria Santos, wa nchini Colombia, ambaye amechanganyikiwa na kuingia na woga baada ya kujifungua mtoto wa ajabu akidai kuwa anapumua moto na kutema cheche.

Ann mwenye umri wa miaka 28, analalamika akieleza
kwamba kichanga chake cha kiume chenye umri wa miezi miwili kuwa ni
mtoto wa shetani.
Ann aliyasema hayo baada ya mtoto huyo kuchoma godoro na nguo kisha kutoweka katika kitanda chake, mahali alipokuwa amemlaza.
Alilalamika kuwa mtoto huyo amekuwa akitengeneza moto na kuchoma vifaa vyake mbalimbali na samani za nyumbani.

Anasema kuwa mtoto huyo pia amekuwa akijibadilisha
mara kwa mara na kuwa na macho ya ajabu yanayowafanya watu kumwogopa
kila wanapomwona.
Ann anasema kuwa wakati mwingine husikia mtoto huyo akicheka kwa sauti za ajabu na kutisha.

Anasimulia kuwa njia mojawapo aliyotumia kusitisha
sauti hizo za ajabu ni kumtaka anyamaze, ambapo mtoto huyo amekuwa
akitii na kukaa kimya.
"Mara nyingi anaweza akapotea tu. Nimemlaza ndani, lakini nikienda kumwangalia nakuta hayupo. Hata nikijaribu kumwangalia simwoni tena, ila ukiondoka, baadaye anarudi na akiamka anaanza kulia kwa sauti. Hapo namchukua na kumpa maziwa,”anasema Ann.
Tatizo hilo limempata Ann kutoka jamii ndogo ya Nueva Estrella, huko Colombia katika ukanda wa Caribbean na kwa kiasi kikubwa jamii ya ukanda huo inaamini ushirikina.
Lakini mama huyo wa watoto watano, anaendelea kumtunza mtoto wake ingawa anakumbana na vikwazo vya mara kwa mara.

Alipozungumza na jarida la The Sun Ann la nchini
Uingereza, Ann alisema: "Huyu ni mtoto wa kishetani. Sijawahi kuona
mtoto kama huyu katika maisha yangu yote, lakini siwezi kumtupa kwani
nimemzaa na nilitunza mimba kwa miezi tisa."
Anasema kuwa mtoto wake aliwahi kupotea kutoka
katika familia yake na kwa wakati huo alikuwa katika kitanda cha mbao,
lakini akaonekana katika mazingira yasiyo ya kawaida.
Mtoto huyo pia amewahi kukutwa katika bakuli, friji, mashine ya kufulia nguo, hata katika begi lililotundikwa ukutani.
"Begi lingeweza kudondoka ikiwa lingewekwa ndizi 20 tu, lakini inashangaza kwa uzito alionao mtoto na begi hilo halikudondoka wala kuonyesha dalili za kujawa kitu kizito,” anasema.
Ann alionyesha kabati na kusema: "Nilimwona ameketi juu ya kabati lile akionekana na ukubwa kama mtoto wa mwaka mmoja. Alikuwa na macho ya kutisha sana pamoja na pembe zilizoota kichwani."

Maelezo ya Ann yanashabihiana na filamu ya ‘The
Omen’ iliyotengenezwa mwaka 1976, ambapo mtoto aliyeitwa Damien alikuwa
na maajabu kama aliyonayo mtoto huyo.
Mtoto huyo alivyoonekana akilia mbele ya mwandishi wa habari huku akitoa sauti ya ajabu, lakini tofauti na maelezo ya Ann, hakuna pembe yoyote iliyoonekana kichwani .

Wenyeji w kijiji anachoishi Ann na mtoto huyo,
mara nyingi wamekuwa wakirusha mawe katika nyumba yake wakimtaka amtoe
nje mtoto wake ili wampoteze, jambo ambalo mama huyo analipinga vikali.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanalalamika wakidai kuwa mama huyo amefuga mauzauza.
Kwa maelezo hayo, huenda Ann akaingia kwenye rekodi mbaya ya unyanyasaji wa watoto kwa kuwa madaktari wanakanusha maneno yake, wakieleza kuwa kulingana na vipimo vya kitabibu, mtoto huyo ni wa kawaida kama walivyo wengine.
Herieth Makwetta kwa msaada wa mtandao.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment