UKWELI wa mambo juu
ya msanii anayependa kulipuka pamba Hemed Suleiman ’Hemedi’ almaarufu
kama PHD au Alejandro, umevuja kwani inadaiwa kuwa nguo zote
anazoonekana anavaa huwa anachukua kwa mkopo na hulipa baada ya muda
fulani lakini sasa kiasi cha fedha anachodaiwa ni kikubwa na hana uwezo
wa kulipa kwa sasa kwani ni zaidi milioni 1.
Duka moja la nguo
maarufu sana lilipo maeneo ya Kinondoni, ndilo lililotoa ishu hiyo baada
kuona jamaa huyo anazingua kulipa na walikuwa wakimpa kila nguo
anayohitaji kwani walimuamini kwa kuwa nguo nyingi alikuwa akinunua hapo
kwao.
Muuzaji wa pamba
hizo katika duka hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe na duka pia,
alisema kuwa awali jamaa alikuwa akilipa kama kawaida lakini ilifika
kipindi alikuwa anachukuwa kila baada ya wiki na hadi hivi sasa anadaiwa
si chini ya milioni 1.
“Hemedi
tunamuamini lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu kiasi cha
fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanya kazi wanahitaji
kulipwa mshahara, tunafikilia kuchukua maamuzi ili aweze kutulipa kwa
haraka. Jamaa sikuhizi haji hapa na wala sijamuona kupita sasa sijui
anakimbia madeni au vipi,” aliongeza
Hata hivyo Hemedi
alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo kama ina ukweli wowote hakuweza
kupatikana na taratibu zinaendelea za kumtafuta ili aweke wazi juu ya
habari hizo.




No comments:
Post a Comment