Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu, akifafanua jambo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi,
amezishukia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), na Bodi
inayoratibu Mfumo wa Uingizaji wa Mafuta Nchini (Pic) kwa kushindwa
kuwajibika katika tatizo la ukosefu wa mafuta.
Alisema hakuna sababu za msingi za kuwepo kwa uhaba wa mafuta ya petroli, dizeli na taa, wakati kuna akiba ya kutosha ya nishati hiyo nchini.
Maswi alisema hayo jana baada ya kuitisha mkutano wa waandishi wa
habari kutoa ufafanuzi kufuatia kukosa mafuta katika mikoa kadhaa nchini
wakati kuna akiba ya zaidi ya lita milioni 83 za mafuta.
Mkurugenzi wa Petroli Ewura, Godwin Samweli, alisema mafuta yapo ya
kutosha, lakini tatizo lipo kwa wenye kampuni zilizopewa leseni za kuuza
mafuta hayo nchini.
“Wenye makampuni wanakataa kuwauzia wenye vituo binafsi mafuta baada
ya kusikia taarifa ya kukwama kwa meli zinazoleta mafuta hayo nchini,”
alisema.
Naye Mkurugenzi wa Pic, Mansoor Hiran, alisema tatizo hilo linatokana
na wakubwa kujiuzia wenyewe na kwamba wao hawana mamlaka ya
kuzilazimisha kampuni zinazonunua mafuta kupeleka mikoani bali Ewura
ndio wenye mamlaka hayo.
Maswi aliiagiza Ewura kuzichukulia hatua za kisheria kampuni zenye
leseni zinazokataa kuuza mafuta kwa wamiliki wavituo vya binafsi.
Alisema mafuta yaliyopo nchini yanatosha kwa matumizi ya siku tano
hadi saba na lita milioni 60.8 zimehifadhiwa kwenye maghala ya TIPER
kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment