Wanajeshi wa Congo mjini Goma
Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
imepuuzilia mbaya makataa iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa
kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji
wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.
Mapema
hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa
serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo
wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabaraza mji wa Goma haikuwa na raia kama
kawaida na magari ya kijeshi na yale ya umoja wa mataifa ndiyo
yaliyokuwa yakizunguka mji huo.
Waasi hao wa M23 wamesema kuwa ikiwa serikali ya
nchi hiyo haitakubali kuanzisha mazungumzo hayo, hawatakuwa na budi ila
kuendelea na mapigano hayo, hadi watakapoiondoa utawala wa sasa.
Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende
amesema waasi hao wanajumuisha wanajeshi ambao wanaungwa mkono na
serikali ya nchi jirani ya Rwanda, ili kuficha vitendo vya kigaidi
vinavyoendeleza katika eneo hilo la Mashariki.
Lakini serikali ya Rwanda imepuuzilia mbali madai hayo, ikisema kuwa hayana msingi wowote
CHANZO: MWANANCHI



No comments:
Post a Comment