Jeshi
la Polisi la Mkoa wa Pwani, linamshikilia Muuguzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Mkuranga, Rehema Gogo (34) kwa tuhuma za kuiba kichanga cha
siku moja.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Phransisco Mwamisi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Ni kweli kichanga hicho kiliibwa na muuguzi wa pale hospitali siku ya Novemba 10, mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi,” alisema Mwamisi.
Alisema muuguzi huyo kwa sasa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi tangu siku ya tukio.
Jeshi la Polisi Wilaya hiyo lilithibitisha kutokea wizi wa kichanga hicho.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa likizo, alikodi gari na kwenda hospitalini hapo na kuingia katika wodi ya wazazi.
“Aliingia wodini humo na kuchukuwa kichanga na kumfunika kwenye hijabu yake. Mama wa mtoto huyo alikuwa ametoka nje kwenda kupiga simu kwao, kwani alijifungua usiku na aliporudi hakumkuta mtoto wake,” alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa jeshi hilo wilayani humo.

CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment