HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Wafanyabiashara Wadaiwa Kuficha Mafuta

UHABA wa mafuta unaotokea hivi sasa nchini, unadaiwa kusababishwa na baadhi ya wafanyabiashara kuficha nishati hiyo kutokana na bei yake kuporomoka katika soko la dunia, wakitegemea watayauza bei ya juu siku za baadaye.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo alisema upungufu wa sasa kwa kiwango kikubwa unachangiwa na hali hiyo.
Kaguo alisema kuna tetesi hizo ambazo na kwamba, ni mapema  kuzizungumzia kwa undani kwa sababu wanafanya uchunguzi zaidi ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua.
Alisema mamlaka haitaki kukurupuka katika suala hilo na uchunguzi ukibaini wafanyabiashara wanaofanya hivyo, itawachukulia hatua kali ikiwamo kuwafutia leseni.
Baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta, walisema Ewura haisemi ukweli.
Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Oil Com kilichopo Boko Magengeni, Ramadhan Mtorwa alisema kauli hiyo haina ukweli wowote.
“Hakuna anayeficha mafuta, bado ninayo na yakiisha yatakuwa yamekwisha, tatizo ni wao wenyewe mfumo wao huu mpya wa kununua mafuta kwa pamoja ndiyo ambao unazua matatizo,” alisema Mtorwa.
Katika Wilaya ya Geita, uhaba wa mafuta umeingia katika siku ya nne mfululizo huku kukiwa na madai kuwa wafanyabiashara wameyaficha ili waweze kupandisha bei baadaye.
 “Juzi na jana kwa vituo vyote kulikuwa na magari yanashusha mafuta hapa, lakini leo wanakwambia hakuna mafuta, sasa kama hakuna hayo waliyoshusha ni nini?” alihoji Sadath Rashid.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Saidi Magalula alisema anavyotambua mkoa wake unayo akiba ya mafuta ya kutosha na amewaonya wanaoyaficha.
Katika Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma uhaba wa mafuta umesababisha kuuzwa a Sh4,000 kwa lita badala ya Sh2,800.
Aisha Ngoma, Pamela Chilongola  na Julius Mathias Dar na Jackline Masinde, Geita, Shakila Nyerere, Kondoa.


CHANZO:MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: