Nape, Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba, Mbando wa Airtel wakisubiri mwili wa marehemu kuwasili nyumbani Lusango Muheza.
Mwili wa Sharo ukiswaliwa.
Nape akimpa pole Zaina Mkieli Mama wa Hussein Ramadhani, Sharo Milionea Kijiji cha Lusanga Muheza Tanga.
Nape (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lilipofika Lusanga, nyumbani kwa marehemu.
Nape akitoa pole za Chama kwenye mazishi hayo.
Nape akitupa udongo kaburini wakati wa mazishi ya Sharo, Lusanga Tanga.
Waombolezaji wakaimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani.
Mzee Kingi Majuto akitupa mchanga kaburini kumzika Sharo.
Nape akitoa pole za Chama kwenye mazishi hayo.
DC wa Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za EOTF ya Mama Mkapa.
Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongo fleva.
Baadhi ya wasanii msibani Lusanga.
Mbando na baadhi ya wasanii.
Vijana wakiwa wamepanda mnazi kuona mazishi ya sharo.
MAELFU ya waombolezaji jana walijitokeza kushiriki mazishi ya
msanii Hussein Ramadhan maarufu kwa jina la Sharo Milionea, huku mamia
wakizirai baada ya kushindwa kujizuia wakati mwili wake unawekwa
kaburini.
Mwili wa msanii huyo ulizikwa jana kijijini kwake Lusanga wilayani Muheza saa 7 mchana, katika tukio lililomshirikisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Waombolezaji walianza kumiminika kijijini Lusanga tangu juzi jioni na idadi yao iliongezeka zaidi jana asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.Sala ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma ambaye baadaye aliamuru jeneza hilo kupelekwa makaburini, ambako waombolezaji kadhaa walipoteza fahamu.
Watu ishirini wapelekwa hospitalini
Miongoni mwa matukio yaliyojitokeza katika msiba huo ni baadhi ya waombolezaji kupoteza fahamu msibani.Matukio tofauti ya watu kuzirai yalitokea wakati mwili wa msanii huyo ulipokuwa unapelekwa nyumbani kwao kijijini Lusanga ukitokea Hospitali Teule ya Wilaya ambako ulihifadhiwa tangu alipopata ajali Jumatatu usiku na wakati wa mazishi.
Miongoni mwa waliopoteza fahamu katika msiba huo ni wasanii na waigizaji wa filamu waliokuwa wakiigiza na Sharo Milionea wakati akiwa katika kundi la AL Riyam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MC wa shughuli hiyo, Steve Nyerere, zaidi ya watu 20 walipoteza fahamu katika msiba huo na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
No comments:
Post a Comment