HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » AJARI IRINGA YAUA WATANO WA FAMILIA MOJA LEO

Gari lililopata ajali ni Toyota RAV 4 T 77 BMP eneo la Tanangozi- Iringa na majina ya  waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali  hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa.
 Baadhi ya akina mama wasamalia wema wa Tanangozi, Iringa wakijaribu kumpepelea mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo
 GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN No. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA  T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO  WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Baadhi ya wasamaria wema wakitoa moja ya maiti kutoka katika gari aina ya Toyota RAV 4 770 BMP huko Tanangozi, Iringa

 Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja  pamoja na mfanyakazi  wa ndani mmoja.
Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la Tanangozi  wilaya ya  Iringa kwenye kizuizi cha barabara  cha mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza  mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4   lenye namba  za usajili T 770 BMP kulipalamia lori  lenye tela kwa nyuma. 

Huku  chanzo kikitajwa  kuwa ni kuendesha  kwa mwendo kasi  wa  dereva  wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke  na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza    kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo kasi na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa  gari hiyo ilikuwa ikitokea  jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.


Hivyo katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba na mama  wa  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao  kufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
 
Waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali  hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa. 

PICHA ZOTE NA MISANJO LIVIGHA (MLALAHOI ALWATAN) WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: