Madaktari wakimhudumia mgonjwa.
DAKTARI wa Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MOI), Deodata Matiko (30) na Muuguzi, Erick
Kimwomwe (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na mashtaka mawili, likiwamo kuomba na kupokea rushwa.
Akisoma hati ya mashtaka jana, Mwendesha Mashtaka
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasamala
alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 15
(1) cha sheria ya Takukuru, sura ya 11 ya mwaka 2007.
Kasamala alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Liwa
kuwa Novemba 27 mwaka huu, katika Taasisi ya Mifupa iliyopo kwenye
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, washtakiwa hao walimwomba Sandford
Harun Mhina, rushwa ya Sh1.5 milioni.
Alidai kuwa washtakiwa hao, walimwomba rushwa hiyo
kama kishawishi cha kumsaidia na kuhakikisha kuwa ndugu yake Fanuel
Daniel Gidion. aliyelazwa katika wodi ya Sewahaji anafanyiwa upasuaji.
Katika shtaka la pili, Kasamala anadai kuwa
Novemba 29 mwaka huu, Matiko na Kimwomwe walipokea rushwa ya Sh1 milioni
kutoka kwa Sandford kwa ajili ya kufanikisha upasuaji huo wa ndugu yake
Fanuel.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote
walikana tuhuma hizo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado
haujakamilika na kwamba hawana pingamizi na dhamana.
Hakimu Liwa aliwaambia washtakiwa hao kuwa dhamana
ipo wazi ma kwamba wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi
katika taasisi zinazotambulika kisheria ambao kila mmoja wao atasaini
bondi ya Sh1.5 milioni.
Pia aliwataka wasitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.
Dk Deodata aliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti hayo ya dhamana huku mwenzake Erick alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo.
CHANZO:MWANANCHI
Pia aliwataka wasitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.
Dk Deodata aliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti hayo ya dhamana huku mwenzake Erick alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo.
CHANZO:MWANANCHI



No comments:
Post a Comment