Mwandishi wa BBC John Solombi
ameripoti kwamba utafiti mpya unaonyesha asilimia 27 ya wanawawake
Tanzania wanafanya ngono kinyume na maumbile.
Mtafiti Mwanasayansi Irene
Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini
Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti
wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia
26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume.
Baadhi ya wanawake kutoka
Kinondoni Dar es salaam, Tanga, Makete na Siha wamekiri kufanya ngono
kinyume na maumbile ambapo Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo
kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia
kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya
mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Amekaririwa akisema “ Utafiti
wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na
kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi,
wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo
hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa
katika utafiti huo”
Wakati wa utafiti huo wanawake
44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana
kinyume na maumbile ambapo Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo
vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete
ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume waliohojiwa wamesema
wanafanya kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna
maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali
ilhali matumizi ya mipira ni hafifu kwani wakitumia mipira (Condom)
inapunguza raha.
Wanawake pia wamedai baadhi ya
tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana akiuolewa na
kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo
hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo
likichukua nafasi.
Watafiti hao wamesema ufanyaji
huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi
na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya
kawaida ya kujamiiana, wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na
maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya
kushindwa kuhimili kusukuma mtoto.
No comments:
Post a Comment