Bunge la Tanzania mkoani Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma, Robert Kitimbo anadaiwa kumtandika vibao ofini kwake,
mtumishi wa Idara ya Afya ya Manispaa hiyo, Mwendwa Mhembano alipokwenda
kudai fedha za kununulia sare.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa
katika tukio hilo ambalo limeripotiwa polisi, mbali na kumpiga,
mkurugenzi huyo alimsukuma na kumwangusha mtumishi huyo na kumsababishia
maumivu.
Imedaiwa kuwa siku ya tukio hilo, Mhembano ambaye
ni muuguzi katika Hospitali ya Makole iliyopo katika Manispaa ya Dodoma,
alifika katika Ofisi ya Mkurugenzi huyo akitaka kupewa ufafanuzi
kuhusu Sh150,000 alizostahili kulipwa kwa ajili ya kununua sare kwa
mwaka.
Baada ya kuingia ofisini kwa mkurugenzi huyo,
ilidaiwa kuwa muuguzi huyo alieleza matatizo wanayopata, ikiwamo ukosefu
wa vifaa na sare za kufanyia kazi, lakini maelezo hayo yalimkera
kiongozi huyo na kuanza kumchapa vibao sambamba na kumkaba shingo na
kumsukuma.
Akizungumza jana mjini hapa, Mhembano alidai
kwamba alipigwa na mkurugenzi huyo na kueleza kuwa tayari suala hilo
alishalifikisha polisi na kufunguliwa jalada DOM/RB/12805/2012.
“Nilikwenda Polisi kutoa taarifa waliniandikia barua ya matibabu (PF3), kimsingi niliumia goti la kulia kwa sababu alinisukuma na nilianguka sakafuni,” alisema Mhembano.
“Nilikwenda Polisi kutoa taarifa waliniandikia barua ya matibabu (PF3), kimsingi niliumia goti la kulia kwa sababu alinisukuma na nilianguka sakafuni,” alisema Mhembano.
Hata hivyo, Mhembano alisema hajui kinachoendelea
baada ya kutoa taarifa hiyo polisi kwani hadi sasa hajaona mkurugenzi
huyo akikamatwa wala kuhojiwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alithibitisha kupokea malalamiko hayo ya Mhembano na kusema kuwa bado anayafuatilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alithibitisha kupokea malalamiko hayo ya Mhembano na kusema kuwa bado anayafuatilia.
“Taarifa hizo tunazo lakini bado tunazifanyia
kazi. Tutakuwa na majibu ya kutosha baada ya kumaliza uchunguzi wetu,”
alisema kamanda huyo jana.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikanusha kumpiga mtumishi huyo lakini akakiri kusikia kile alichokiita uvumi huo, kwa watu.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikanusha kumpiga mtumishi huyo lakini akakiri kusikia kile alichokiita uvumi huo, kwa watu.
Alisema Mhembano alifika ofisi kwake Novemba 24,
mwaka huu saa za jioni akiwa amelewa na kuanza kumtukana, akidai sare
kwa nguvu... “Niliamua kuondoka ofisini na kumwacha,” alisema na
kuongeza: “Mimi ni mtu mzima, siwezi kumpiga mtu kama yule na hakuna mtu
anayeruhusiwa kumpiga mwenzake. Yeye alikuja ofisini kwangu akiwa
amelewa chakari na kuanza kunitukana, akidai sare. mimi nikaamua
kumkimbia lakini nashangaa anazusha kuwa nilimpiga,” alisema Kitimbo.
Mkurugenzi huyo alisema baada ya tukio hilo,
Mhembano alielekezwa na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), kuandika barua ya
maelezo, lakini hajafanya hivyo hadi sasa.
Alipotakiwa kuzungumzia madai ya mkurugenzi huyo kwamba alikwenda ofisini kwake akiwa amelewa, mama huyo alijibu: “Siyo tu siku hiyo, mimi sijawahi kuonja wala kunywa pombe hata siku moja katika maisha yangu.”
MWANANCHI

No comments:
Post a Comment