Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa
Wilaya mpya ya Kalambo alipotembelea hivi karibuni kuona jengo ambalo
Mkuu wa Wilaya hiyo atalitumia kama ofisi yake ya muda. Aliwataka
viongozi pamoja na watumishi kutoweka urasimu mbele katika utendaji kazi
na badala yake kuwa kitu kimoja bila kujali cheo cha mtu. "Kila mmoja
atekeleze jukumu lake katika eneo lake na kwa kufanya hivyo kutaifanya
Wilaya hii nzuri kusonga mbele kwa kasi, kwa watumishi wa kada za chini
mnatakiwa kumuona Mkuu wa Wilaya kama rafiki na kumuona muda wowote pale
ushauri wake unapohitajika" alisema Injinia Manyanya.
Kushoto
na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
alipotembelea kuona hali ya ofisi hiyo, Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo
machachari ndugu Moshi Mussa Chang'a. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka
viongozi hao kuhakikisha suala la mipango miji bora linazingatiwa katika
kupanga miji na wilaya kwa ujumla.
Mazungumzo yakiendelea, hata hivo Mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba viongozi hao kuwa wavumilivu kwani kutokana na changamoto
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akielezea baadhi ya kero zake
kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Mkuu huyo wa Mkoa
aliwapa moyo kuwa watumie uwezo wao mdogo walionao kutatua baadhi ya
kero hizo na nyingine watashirikiana kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Picha
ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na
viongozi pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo.
Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Moshi Chang'a.
Jengo ambalo linatumika kwa muda kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo.
Makazi ya muda ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
PICHA NA OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA










No comments:
Post a Comment